Monday, April 13, 2020

TAMTHILIYA YA NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE

TAMTHILIYA: NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE
MTUNZI: EDWIN SEMZABA
MCHAPISHAJI: THE GENERAL BOOKSELLERS LTD
CHAPA YA 1-1988
UTANGULIZI
Ngoswe-penzi Kitvu cha Uzembe  inaonyesha namna jamii inapaswa kushiriki mipango mbalimbali ikiwepo ya kisiasa kiuchumi na kiutamaduni.Mafanikio ya mipango hiyo inategemea na kujulikana kwa idadi ya watu utayari,uelewa wa watu hao kuhusu mipango husika Tamthiliya hii inaonyesha kazi ya kuhesabu watu ilivyokwama kijijini kwa mzee mitomingi ngengemkeni kutokana na uzembe wa afisa wa kuhesabu sensa Ngoswe.
DHAMIRA
 MAPENZI
Mwandishi Edwin semzaba ameonyesha jinsi mapenzi yalivyo kitovu cha uzembe,wahusika Ngoswe na Mazoea wametumiwa na mwandishi kufafanua dhamira hii Ngoswe baada ya kufika kwa mzee Mitomingi anashindwa kuitawala nafsi yake mara anapomuona Mazoea,Ngoswe aliamua kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na Mazoea hali iliyomfanya ashindwe kuimudu kazi yake na mapenzi kwa wakati mmoja.Ngoswe anamtorosha Mazoea kitendo hiki kinamuudhi balozi Mitomingi Ngengemkeni (baba mzazi wa mazoea)na kuamua kuchoma moto karatasi muhimu za serikali.Ngoswe anaonekani ni mzembe kwa kuwa alishindwa kutofautisha kazi na mapenzi kama msomi (afisa wa sensa) alitakiwa ajue umuhimu wa kazi iliyompeleka kijijini.
 ULEVI NA ADHARI ZAKE
Katika tamthiliya ya ngoswe penzi kitovu cha uzembe mwandishi anaonyesha namna ulevi ulivyoleta madhara,mfano kuchelewesha kazi.Wahusika Mitomingi na Ngoswe wanashindwa kukamilisha kazi kwa vile wahusika (wahesabiwa)wapo kwenye Pombe kama maneno haya yanavyothibitisha;
Mitomingi:Haya ni matatizo yote hii shauri ya pombe nadhani yupo kilabuni
Ngoswe: hawezi kwenda kuitwa?
Mitomongi: haitosaidia mkewe tu hana habari ya kuhesabiwa sembuse hao wengine kwa leo haitowezekana Licha ya kuchelewesha kazi ulevi huaribu kazi.Mfano:ngoswe anaunguza karatasi za sensa baada ya kulewa pombe ya mnazi.
ELIMU
Elimu ni chombo cha ukombozi kama itatumiwa vizuri ipaswavyo,mwandishi wa tamthiliya hii amemuonyesha kijana Ngoswe (msanii)alivyoshindwa kutumia elimu yake hususani katika kujua namna ambavyo  maisha ya mjini yanavyotofautiana na maisha ya kijijini,Ngoswe anajikuta akiharibu kazi yake kwa kukosa maarifa. Mwandishi ameonyesha elimu katika familia ya mito mingi haikupewa thamani yoyote ile wananchi wengi hawakuwa na elimu kwa kisingizio cha shule kuwa mbali, ukosefu wa elimu ulichangia ukosekanaji wa huduma muhimu kama vile hospitali ,miundo mbinu na maji ili kupata maendeleo,suala la elimu lazima litiliwe maanani watu wakieleweshwa wataweza kujua wajibu wao :- Mfano:kujali kazi na kuacha ulevi “kutumia vema hospitali badala ya kutegemea mitishamba
 UCHAWI NA USHIRIKINA
Mwandishi wa tamthiliya hii ameonyesha jinsi watu wengi ndani ya jamii walivyo na imani juu ya uchawi,wanajamii hawa wameweka vikwazo kuhusu sensa wakiamini kuwa mtu anayewahesabu wenzake ni mchawi. Mfano:mama anasema mchawi ndiyo huhesabu watoto wa wenzake ili awaroge sasa wewe ni mchawi?hata kama si mchawi siwezi kukubali unihesabu maana sijui nia yako kama ni mbaya au nzuri.Imani hizo ni za kishirikina zinachangia kukwama kwa zoezi la sensa pia maendeleo kwa ujumla kuwachini,watu wakiugua hawapelekwi hospitali badala yake wanapelekwa kwa mganga wa kienyeji wakidhani kuwa amerogwa.
5. NAFASI YA MWANAMKE
Katika tamthiliya hii mwanamke ametazamwa katika mitizamo tofauti kama ifuatavyo;
Mwanamke amechorwa Kama chombo cha starehe, mwandishi amemuonyesha mzee mitomingi kuwa na wake wengi (mitala) bila kuoyesha bayana kazi zao.
Mwanamke amechorwa kama mtu asiye na sauti .mfano: Mazoea na mama yake hawakushirikishwa katikamipango ya kutaka kuolewa mazoea kwa vile walionekana hawana mchango wowote katika maamuzi hayo
Mwanamke amechorwa kama mlezi, katika tamthiliya hii inamchoramwanamke kama mtu mwenye majukumu ya malezi ya watoto, baada ya Mazoea kuwa namahusiano na Ngoswe mzee Mitomingi anamlaumu mama yake Mazoea kuwa hakuona dalili ya mahusiano ya kimapenzi kwa kuwa ni jukumu la mama kumwangalia binti yake.
NDOA NA MALEZI
Mwandishi wa tamthiliya hii ameonyesha suala la ndoa ni sualala hiyari na si kufuata matakwa ya wazazi, Mazoea alichaguliwa mchumba na wazazi wake (baba yake)hali iliyomfanya kutoroka na ngoswe Hali kadhalika katika tamthiliya hii wanaume wengi wana mke zaidi ya mmoja hali hii inapelekea familia kuwa kubwa na kushindwa kuzitunza. Mfano: Mzee Mitomingi ana wake wawili ambao ni mama Mazoea na mama Mainda, wazazi hawa wanatofautiana katika malezi hasa kwa Mazoea hali iliyopelekea kuwa na tabia mbaya.  Kwa upande mwingine ndoa zenye mke zaidi ya mmoja haziwi na upendo ndani ya familia hivyo kuwa kikwazo kwenye malezi.
UVIVU NA ATHARI ZAKE
Wanakijiji wa Ngengemkeni mitomingi wengi ni wavivu muda mwingi wanautumia kwenye ulevi na uvuvi, unawafanya wakose huduma muhimu kama shule, barabara na hospitali huduma hizi zingepatikana kama wananchi wenyewe wanajitolea. Siku zote wavivu wanatafuta visingizio, vifo vingine vinatokea sababu ya uzembe na uvivu kisha sababu hutafutwa. Mfano:wanawake wawili walidai mume wao amerogwa ili hali wenyewe hawakumpeleka hospitali
 MIGOGORO
Ni hali ya kutoelewana baina ya pande mbili zenye mitazamo tofauti Katika tamthilia ya Ngoswe penzi kitovu cha uzembe kuna migogoro mingi ambayo imeweza kujitokeza Kama ilivyoonyeshwa na mwandishi
Mgogoro kati ya Ngoswe na wazazi wa Mazoea
Chanzo cha mgogoro huu umetokana na Ngoswe kumtorosha Mazoea, suluhisho wazazi kumfukuza Ngoswe na Mazoea kuchoma karatasi na kumwadhibu Mazoea.
Mgogoro kati ya Mazoea na wazazi wake
Chanzo cha mgogoro huu ni baada ya Mazoea kutoroka na Ngoswe ili hali Mazoea tayari ana mchumba wake, suluhisho ni mitomingi kumchapa mazoea na kuchoma karatasi za sensa.
Mgogoro kati ya Ngoswe na serikali,
Chanzo cha mgogoro huu ni Ngoswe kuharibu kazi ya sensa na hivyo kusababishia serikali ishindwe kupanga mipango ya maendeleo, suluhisho halijapatikana hadi mwisho.
UJUMBE
Si jambo zuri kuchanganya suala la kazi na starehe au mapenzi,wakati wa kazi uwewa kazi na wakati wa starehe uwe wa starehe
Wavulana wanaovuruga wasichana siku moja watakamatwa na wasichana wenyewe wanapewa tahadhali wasiwe na maamuzi bila kufikilia.
Elimu ni kitu cha muhimu sana katika jamii na jamii isipokuwa na watu walioelimika hawawezi kuwa na maendeleo maana ili tuwe na maendeleo tunatakiwa tutupilie mbali ulevi na uvivu katika jamii yoyote
Uchawi na ushirikina ni kikwazo kikubwa katika maendeleo

FALSAFA
Mwandishi anaamini kuwa ni rahisi jamii kuingia kwenye matatizo kama itachanganya mambo mengi kwa wakati mmoja hivyo ikumbukwe kuwa kila jambo na wakati wake.
MUUNDO
Muundo uliotumika katika tamthiliya ni wamuundo wa moja kwa moja ambapo kazi nzima ipo katika sehemu tano ambazo mwandishi amezipa majina ya kitwasira kulingana na ukubwa wa tatizo linalozungumziwa ,yaani ameonyesha kuingia kwa Ngoswe kijijini mazingira yanayoashiria hali ngumu ya maisha.
MTINDO
Mtindo uliotumika ni wa kidayalojia ambapo wahusika wake wanazungumza kwa kujibizana Pia kuna matumizi ya nafsi zote tatu na nafsi hizo zimetumika katika sehemu mbalimbali.Mfano sehemu ya tano kwa matumizi ya nafsi ya kwanza pale Ngoswe anapoulizwa na serikali kuhusu takwimu akajibu “usemi sinao”
MANDHARI
Kitabu hiki kimejengwa katika mandhari ya kijijini,hii inadhihirishwa na ukosefu wa huduma muhimu kama vile shule hospitali na miundo mbinu. Tabia za wahusika pia zinaonyesha mandhari ya kijijini mfano, ulevi wa pombe za mnazi,watu kutojali elimu,kun’gan’gania mila zilizopitwa na wakati



MATUMIZI YA LUGHA
Mwandishi ametumia lugha nyepesi na yenye kueleweka pia mwandishi ametumia tamathali za semi,misemo na mbinu nyingi za kisanaa.
Tamathali za semi.
Hizi ni semi au kauli zitumiwazo na mwandishi katika kazi ya fasihi ili kuongeza ladha katika kazi husika
Tashibiha
Ni tamathali ilinganishayo vitu viwili au zaidi kwa kutumia viunganishi kama mithili ya, kama, mfano wa kwa Mfano,
Ngoswe anaposhangaa ardhi ya kijijini kwa balozi Mitomingi anasema Udongo mwekundu kama ugoro wa sabiani
Tazama suruali yake kama kengele ya bomani
Nikitoka hapa najitupa kitandani kama gogo
Tafsida Ni tamathali itumiwayo kupunguza ukali wa maneno. Mfano Mainda anasema labda anajisaidia (UK 21)
Takriri ni tamathali inayorudiarudia neno ili kuweka mkazo juu ya kile kinachosemwa Mfano; karibu, karibu (pale Ngoswe alipokuwa akikaribishwa)
Mdokezo Ni tamathali ambayo hueleza jambo kwa kukatakata maelezo Mfano Mazoea anasema sijui……sijui……siwezi namwogopa baba (Uk 22)
Tanakali za sauti Ni tamathali inayoiga mlio wa vitu mfano Ngoswe alishindwa kujizuia akacheka ha ha ha ha
Methali
Ngoswe anamwambia Mazoea v  “Penye nia pana njia” (uk 22)
Misemo
Hebu keti tutupe mawe pangoni
 Kupeleka chakula ndio unafanya makambi
WAHUSIKA
Wahusika ni watu walioshiriki katika mchezo au tamthiliya husika. 
NGOSWE
Ni msomi anayependa kazi ya kuhesabu watu lakini kutokana na tamaa ya mwili wake anaharibu kazi baada ya takwimu zote kuchomwa moto na Mitomingi kutokana na kitendo cha kujaribu kumtorosha mazoea .
Mazoea
Ni Msichana mwenye umri wa miaka 18-20. Ni motto wa balozi (Mitimingi). Anawakilisha   wanawake wasio na msimamo katika mapenzi

Ngengemkeni mitomingi
Huyu ni balozi. Ni  Baba yake Mazoea Anachoma karatasi za takwimu kutokana na Ngoswe kutaka kumtorosha Mazoea. Ni mzee aliyeshikilia ukale na anapenda ndoa za mitara.
JINA LA KITABU
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe jina hilo la kitabu linasadifu yaliyomo ndani ya kitabu, kwani msanii kwa kiasi kikubwa amejaribu kujadili na kuonyesha matatizo yanayoikumba jamii katika shughuli za kijamii,matatizo hayo ni kama uchawi ulevi uzembe na dhana nyingine potofu.
KUFAULU NA KUTOFAULU KWA
MWANDISHI
 Mwandishi katika tamthiliya hii amefeli kwa kuwa ameonyesha matatizo yaliyomo katika jamii bila kuonyesha mbinu mbadala ya kuyatatua.

No comments:

Post a Comment

Maswali ya vitabu na majibu yake

 NECTA 2012 “Washairi ni wataalamu wazuri na waliobobea katika kutumia taswira zinazotoa ujumbe kwa jamii.” Tumia taswira tatu kwa kila diwa...