Sunday, April 12, 2020

Eleza ni kwa vipi kategoria ya kileksika inaingiliana na kategoria ya tungo huku ukitolea mifano hai kutoka lugha ya Kiswahili, kiingereza na nyingine moja ya kibantu


SWALI: Eleza ni kwa vipi kategoria ya kileksika inaingiliana na kategoria ya tungo huku ukitolea mifano hai kutoka lugha ya Kiswahili, kiingereza na nyingine moja ya kibantu

UTANGULIZI
Dhana ya kategoria imejadiliwa kwa namna tofauti tofauti.
Khamis na Kiango (2002) wameigawa kategoria katika mitazamo miwili wanamapokeo na wanausasa. Ambapo wanamapokeo walitumia dhana ya kategoria kumaanisha sifa bainifu zinazoambikwa kwenye aina za maneno kama vile nafsi, idadi, njeo, dhamira, na ngeli. Wakati wanausasa wanaona kuwa kategoria ni zile aina za maneno kama vile Nomino (N), vivumishi (V), vielezi (E), viunganishi (U), vitenzi (T), viwakilishi (W), na Kihusishi (H).
Massamba (2009) anaeleza kuwa kategoria ni jumla ya maumbo, faridi au vipashio vingine ambavyo huchangia sifa fulani au ambavyo viko katika kiwango kimoja.
Samwel (2) anaeleza kategoria kwa mtazamo wa kisarufi mamboleo kuwa ni darajia mbalimbali katika uundaji wa tungo. Anaendelea kueleza kuwa kuna kategoria za darajia mbili ambazo ni kategoria ya neno (kileksika) na kategoria ya virai. Ambapo kategoria ya kileksika huhusika na aina mbalimbali za maneno kama vile nomino, vivumishi, viwakilishi, vielezi, vitenzi, viunganishi, vihusishi na vibainishi.
Kwa ujumla kwa kurejelea mtazamo wa sarufi mamboleo kategoria ni jamii au makundi yanayofanya kazi kwa kufanana na yenye sifa zinazofanana.
Naye O’Grady (1996) katika kufafanua kategoria za kileksika anaona kuwa ni kategoria za kiwango cha neno moja moja na anataja aina nne za maneno ambazo ni nomino, kivumishi, kitenzi na kielezi.
Massamba (2009), anatoa maana ya kategoria ya kilekisika kwa kusema kuwa ni jumla ya maumbo, faridi au vipashio vingine ambavyo huchangia sifa fulani au ambavyo viko katika kiwango kimoja. Maana hii ni ya jumla kwani imeeleza dhana ya kategoria ya kileksika kwa ujumla bila kujikita katika kategoria za miundo ambayo ndiyo sintaksia.
 Kategoria za kileksika katka lugha ya kiswahili zipo kategoria nane za kileksika ambazo ni nomino, vitenzi, viwakilishi, vielezi, viunganishi, vivumishi, vihusishi na vihisishi.
 Kwa mujibu wa Massamba, Kihole, Hokororo (2012), wanasema tungo ni nomino ambayo imetokana na kitenzi tunga ambacho kina maana kushikanisha vitu kwa pamoja kwa kutumia kitu Kama uzi, ungwe ndani yake. Hivyo katika taaluma ya sarufi neno tungo lina maana ya kuweka au kupanga vipashio sahihi ili kujenga vipashio vikubwa katika tungo. Katika lugha ya kiswahili Kuna aina nne za tungo ambazo ni tungo neno, tungo kirai, tungo kishazi na tungo sentensi ambapo tungo hizo huundwa na aina mbalimbali za maneno Kama nomino, kiwakilishi, vivumishi,viunganishi,vitenzi,vielezi,vihisishi na vihusishi.                                               
Kamusi ya kiswahili (2014), tungo ni kipashio cha kimuundo kipatikanacho kwa kuunganisha vipashio sahihi kuweza kupata kipashio kikubwa zaidi, kwa ujumla tungo ni kipashio cha kimuundo ambacho huwekwa pamoja ili kujenga vipashio vikubwa zaidi katika sarufi.
 Kategoria za kileksika na kategoria za tungo ni kweli zina mipaka inayo pitika kwa sababu tungo hujidhihilisha katika miundo minne ambayo ni tungo neno, tungo kirai, tungo sentensi na tungo kishazi. Viwango hivi ndivyo vinavyodhibitisha kupitika kwa kategoria za kilekisika na kategoria za tungo katika lugha.
Kategoria ya kileksika hubainisha kujua aina mbalimbali za virai pamoja na miundo yake, Massamba na wenzake (2012) wanaeleza kuwa miundo ya virai hukitwa katika aina za maneno ambazo ndizo chimbuko la mahusiano maalumu ndani ya vipashio hivi. Mfano wa virai hivyo ni KN, KV, KE, KT na KU.
Mfano wa Virai katika lugha ya Kiswahili
Kirai Nomino(N) mtoto, Juma, Arusha, KV ni mbishi, mbaya, mzuri na KE ni pole pole, taratibu, asubuhi, leo.
Katika lugha ya kiingereza
John /kicked /the ball
NP         VP      NP
Katika lugha ya kibantu ya kiyao
Lizimba /lipitile
   KN        KT
Kategoria hubainisha kujua aina za maneno katika lugha husika na dhima zake katika tungo, Wesana-Chomi (2003) anaeleza kuwa maneno ya lugha hufanya kazi mbalimbali katika tungo. Mfano kuna maneno yanayofanya kazi kuonesha nani katenda tendo, nani katendewa tendo au nani katendwa tendo. Maneno yenye kazi hizo katika tungo huitwa nomino. Pia, maneno mengine hutoa taarifa juu ya nomino na maneno hayo ni kivumishi. Aidha, maneno mengine hutaja tendo au jambo lifanywalo na mtenda tendo na maneno hayo huitwa vitenzi. Kwa mfano;
Mwalimu anafundisha
     N              T
Mtoto mzuri
   V       
Hivyo katika mifano hii neno Mwalimu ambalo ni nomino limesimama kama mtenda wa jambo na katika mfano wa pili neno mzuri limesimama kama kivumishi ambacho kinatoa sifa juu ya nomino. Hivyo kategoria husaidia kujua aina za maneno.
Kategoria ya kileksika hubainisha miundo ya sentensi katika lugha,kategoria za kileksika  hubainisha  kwamba muundo wa sentensi huelezwa kwa kutaja kategoria za maneno yanayounda sentensi hiyo. Hivyo kategoria za maneno husaidia kujua miundo mbalimbali ya sentensi kwani kuna sentensi zenye
Katika lugha ya Kiswahili
muundo wa (N + T) yaani Nomino na kitenzi,
Mtoto anakula
   N       T
Katika lugha ya kiingerza (N +T)
Juma /plays
  N       T         
Katika lugha ya kibantu ya kiyao Muundo wa (N +T)
Mbuzi/ jiwile
   N        T
Hivyo mifano tajwa hapo juu dhahiri inaonesha namna kategoria ya kileksika ilivyotumika katika kuonyesha miundo ya sentensi.
Kategoria ya kileksika hubainisha  katika utungaji wa sentensi, O’Grady (1996) anaeleza kuwa neno fulani liko katika kategoria fulani kutokana na linavyofasiliwa, mfano nomino hutaja vitu, vitenzi ni maneno yanayotaja vitendo, vivumishi ni maneno yanayotaja sifa za nomino na vielezi ni maneno ambayo hueleza namna tendo linavyofanyika. Hivyo kutokana na maelezo hayo ni wazi kuwa mwanagenzi anapotaka kutunga sentensi ni lazima ajue kategoria za maneno kwani hawezi kutunga sentensi pasipo kuhusisha kategoria za maneno.  Hivyo kategoria husaidia katika utungaji wa tungo mbalimbali katika lugha husika. Kwa mfano;
Wanafunzi wanasoma
     N                 T
Mtoto anacheza mpira
   N            T         N
Baba analima na mama anafua nguo
N        T       U    N       T        N
Hivyo mifano ya juu inaonesha namna kategoria za kileksika  zilivyotumika katika kuunda ama kutunga sentensi mbalimbali.
Kwa kuhitimisha kategoria za tungo na kategoria za kileksika zote zinategemeana bila tungo hapawezi kuwa na maneno na bila maneno hatuwezi kuunda tungo hivyo kategoria za kileksika na kategoria za tungo zote zina saidia kuonesha uchunguzi sahihi wa maneno na uteuzi wa tungo sahihi katika lugha yoyote ulimwenguni iwe kiswahili, kireno n.k, aina za maneno ndizo zinaamua tungo ipewe jina gani inaweza ikawa sentensi, kirai, kishazi, na neno hivyo kupitia kanuni mbalimbali za kisarufi ndipo tunapata kupitika huko Kati ya kategoria za kileksika na kategoria za tungo Kama tungo neno, kirai, kishazi na sentensi.

MAREJELEO.
TUKI, (2004), Kamusi ya Kiswahili Sanifu Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Massamba na Wenzake (2012), Sarufi ya kiswahili sanifu (samakisa) Sekondari na Vyuo  Dar es salaam.
Ndugu, A E, bubwa, H,N, mirkau, S.A, (2014), Kamusi teule ya kiswahili, Nairobi, Kampala, Dar es salaam,Kingali.
Kiwere A.D, (2007) Ukuaji wa Kiswahili na ustawi was Jamii ya wazungumzaji wake Dar es salaam.
Besha, R.sM (2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu. Dar es Salaam: Dar es Salaam University                                    Press.
Massamba, D na Wenzake. (1999) Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu,Sekondari na vyuo. Dar es                               Salaam: TUKI.

No comments:

Post a Comment

Maswali ya vitabu na majibu yake

 NECTA 2012 “Washairi ni wataalamu wazuri na waliobobea katika kutumia taswira zinazotoa ujumbe kwa jamii.” Tumia taswira tatu kwa kila diwa...