UUNDAJI WA MANENO
Uundaji wa maneno ni shughuli ya kuunganisha viambajengo (vipashio) mbalimbali ili kupata maneno tofauti yenye maana mbalimbali ambazo ni kamili.
Kwa kuwa maendeleo ya jamii hubadilika, hukua na kuongezeka hivyohivyo lugha nayo hukua na kubadilika kwa lengo la kukidhi haja ya mawasiliano.
Ili msamiati uongezeke lazima maneno yaundwe kwa lengo la kuboresha mawasiliano kulingana na wakati uliopo.
UMUHIMU WA UUNDAJI WA MANENO
Kupata msamiati wa kutosha katika lugha husika ili kukidhi mabadiliko yanayojitokeza.
Kukabiliana na suala la maendeleo ya sayansi na teknolojia katika ongezeko la maneno mapya.
Ubunifu wa maneno mbalimbali hutokana na njia mbalimbali kama vile uambishaji wa maneno, kubadili mpangilio wa herufi kutohoa maneno ya lugha nyingine, kuambatanisha maneno, kufananisha sauti, umbo, mlio.
UUNDAJI WA MANENO KWA KUTUMIA MOFIMU=
(a) MOFIMU
Maana
Mofimu ni kipashio kidogo chenye maana ya kisanifu na kileskia, kipashio hicho kinaweza kuwa sehemu ya neno au neno zima.
- Tu – ta- pi – ka
- U – som – i
Katika Kiswahili, mofimu inaangaliwa katika daraja la vipashio vya lugha. kipashio hiki hakiwezi kuvunjwavunjwa zaidi bila kupoteza maana..
AINA ZA MOFIMU
Kuna aina kuu mbili za mofimu
(i) Mofimu huru (sahihi)
(ii) Mofimu tegemezi
MOFIMU HURU/ SAHIHI
Ni mofimu inayoweza kusimama peke yake na kuweza kutumiwa katika tungo bila kuwa na kiambishi chochote. Mofimu huru zina hadhi ya neno na zinaweza kuwa aina yoyote ya neno kama vile: -
- Majina (nomino): juma, simba, baba, mama, dada, kaka
- Viwakilishi: mimi, sisi, yeye, wao, ninyi
- Vivumishi: safi, chafu, kile, refu
- Vitenzi: Sali, tafiti, jibu
- Viunganishi: na, hata, hadi
- Vielezi: haraka , polepole, sana, mno
MOFIMU TEGEMEZI
Ni mofimu zinazofungamana na mofimu nyingine na zinapotumika hutegemeana ili kueleza dhana iliyokusudiwa. Mofimu hizi zinapofungamana huunda neno. Mofimu zinazounda neno huweza kuwa mbili au zaidi kulingana na mchangamano wa dhana ulio katika neno linaloundwa
Mfano:
Mtoto - m- toto
Watacheza - wa – ta – chez – a
Anasoma - a – na – som –a
Mkulima - m – ku – lim –a
NAFSI
Nafsi katika umoja nafsi katika wingi
(i) mimi NI sisi TU
(ii) wewe U ninyi M
(iii) yeye A wao WA
Mfano:-
Neno “analima” lina mofimu nne (4) ambazo hufungamana na kujenga neno “analima” kila moja ya mofimu hizi isimamapo peke yake haina maana yoyote isipokuwa ina maana kisarufi ambayo humuwezesha mwanaisimu kuchambua maana ya mofimu hiyo.
Analima - a – na- lim – a
A – kiambishi awali kipatanishi cha nafsi ya III umoja
Na – kiambishi awali cha wakati uliopo
Lim – mzizi wa neno
A – kiambishi tamati
Dhima kuu ya mofimu ni kuongeza msamiati. Msamiati huo unaweza kuongezeka kwa kuunda neno zima. Pia msamiati unaweza kuundwa kwa shina moja kwa kuweza kuunda na kutoa maneno yenye maana mbalimbali.
Mfano:-
Neno “cheza” linaweza kuwa : mchezaji, mchezo, wanachezea, tulicheza, uchezeshaji, alimchezesha n.k.
Vilevile mofimu tegemezi zina dhima mbalimbali tofauti na uundaji wa msamiati. Baadhi ya dhima hizi ni kama vile,
kudokeza nafsi
kuonesha njeo (wakati)
kuonesha/ kudokeza urejeshi
kudokeza ukanushi
kudokeza kauli mbalimbali
(b) UUNDAJI WA MANENO KWA KUTUMIA UAMBISHAJI
(i) Maana
- Uambishaji ni kitendo cha kupachika kiambajengo (mofimu) cha neno kwenye mzizi wa neno ili kukamilisha muundo wa neno
VIAMBISHI
- Viambishi vinavyowekwa kwenye mzizi wa neno na kukamilisha muundo wa neno hilo. Viambishi vinaweza kuambilishwa kabla au baada ya mzizi wa neno (kiambishi kinaweza kupachikwa mwanzoni na mwishoni mwa mzizi wa neno ). AU
- Viambishi ni mofimu muhimu sana katika uundaji wa maneno mapya kutokana na mzizi wa neno moja. AU - Viambishi ni mofimu zinazowekwa kwenye mzizi wa neno na kukamilisha muundo wa neno.
Kwa mfano neno: ANAYEJIPIKIA
Viambishi awali (mwanzoni) vyake ni A – NA- YE – JI
Viambishi tamati ni –I – A – na mzizi wa neno hilo ni – PIK-
AINA ZA VIAMBISHI
(a) Viambishi awali
- Hivi ni viambishi vinavyowekwa kabla ya mzizi wa neno navyo ni vitano
(ii) Viambishi ngeli
Mfano:
M – tu = wa – tu
M – ti = mi – ti
M – zuri = wa – zuri
M – safi = wa – safi
(iii) Kipatanishi (kiambishi awali cha nafsi)
Hivi hujitokeza katika vitenzi na wakati fulani huitwa viambishi awali vya nafsi
Mfano: - Umoja Wingi
Ni – nalima tu – nalima (nafsi 1)
U – nalima m – nalima (nafsi 2)
A – nalima wa – nalima ( nafsi 3)
(iv) viambishi awali vya wakati (njeo)
Hivi huonesha wakati tendo limefanyika katika kitenzi
Mfano: analima
A – na- lima (wakati uliopo)
A – li – lima (wakati uliopita)
A – ta – lima (wakati ujao)
(v) Viambishi awali vya hali
Hivi huonesha hali mbalimbali katika kitenzi
Mfano: -
Hu – lima (hali ya mazoea)
A – me – lima (hali timilifu)
A- nge – lima ( hali ya masharti)
(vi) viambishi awali vya rejeshi vya mtendaji wa jambo au tendo (kiima)
Hivi hutaja mtenda wa jambo
Ni – na- ji – kata
A – na – ye – sema
U – li – o – enea
(vii) Viambishi awali rejeshi vya mtendwa
Hivi hutaja mtendwa wa jambo
Mfano: -
Tuli – u – panda
Nina – i – soma
Ana – m – piga
Wana – ni – soma
(viii) Viambishi awali vikanushi na yakinifu
Hivi huwekwa katika kitenzi ili kukamilisha hali ya kukanusha, viambishi vya kukanusha katika lugha ya Kiswahili ni ha – hu – na – si
Mfano: -
U – naimba hu – imbi
Ni – nacheza si – chezi
A – naimba ha- imbi
(b) Viambishi kati
Ni viambishi vinavyopachikwa ndani ya mzizi wa neno na hivyo kuukuta katika sehemu mbili. Viambishi kati havitokei katika Kiswahili lakini vipo katika sehemu nyingine, mfano kiebrania.
(c) Viambishi tamati
Hivi ni viambishi vinavyoambishwa baada ya mzizi wa neno navyo ni vya aina mbili.
(i) Viambishi tamati maana
Hivi hutokea baada ya mzizi wa kitenzi bila kubadilisha umbo la mzizi wenyewe. Viambishi tamati maana hutaja maana au dhana.
Mfano: -
Lim –a
Lim – wa
Chez – a
Chez – wa
(ii) Viambishi tamati vijenzi
Hivi ni viambishi vinavyoandikwa baada ya mzizi wa kitenzi viambishi tamati vijenzi navyo hutokea mara baada ya mzizi wa kitenzi na vina kazi kuu nne.
(a) Kuleta maana ya ziada ya kule kwenye maana ya asili iliyobebwa na mzizi wa kitenzi.
Mfano: -
Lima – limia- limika – limisha – limiwa
Tendo – tendea – tendeka – tendesha – tendewa
(b) Kujenga mzizi mpya wa kitenzi ambao utabebeshwa maana ya asili ya kitenzi na maana ya ziada. Mzizi huu mpya huitwa “mzizi wa mnyambuliko”
Mfano: -
Kitenzi
Mzizi asilia
Mnyambuliko
Mzizi wa mnyambuliko
Piga
Pig -
Pigana
Pigan
Cheza
Chez -
Chezeka
Chezek
Imba
Imb -
Imbisha
Imbish
Ruka
Ruk -
Rukiana
Rukian
Lima
Lim -
Limika
limik
(d) Huweza kubadili neno toka aina moja na kuingia aina nyingine
Mfano: -
Omba – ombeana – ombaji – ombeka – ombi – ombeaji
T T N T N T
(e) Kuweza kuzalisha kauli mbalimbali za tendo kama ifuatavyo;- Kauli ya kutenda;- Chez – a Chek – a
Imb – a
Kauli ya kutendwa;- Chez – wa
Chek – wa
Imb – wa
Kauli ya kutendeka;- Chez – ek – a
Chek – ek – a
Imb – ik – a
Kauli ya kutendewa;- Chez – ew –a
Chek – ew – a
Imb – iw – a
Kauli ya kutendea Chez –e –a
Chek – e – a
Imb –i –a
Kauli ya kutendeana Cheze – an – a
Cheke – an – a
Imbi – an – a
Kauli ya kutendesha Cheze – sh – a
Cheke – sh – a
Imbi – sh – a
(a) MZIZI KIINI CHA KITENZI
Mzizi au kiini ni ile sehemu ya neno inayobakia baada ya kuondolewa aina zote za viambishi yaani viambishi awali na tamati (mzizi ni sehemu isiyobadilika).
Kuna aina mbili za mzizi
(i) Mzizi asilia
Huu ni mzizi unaobakia baada ya kuondolewa viambishi tamati vijenzi. Mzizi huu mpya hubeba maana ya ziada ya hivyo viambishi maana kama vile:
NENO MZIZI ASILIA
Lima lim-
Lewa lew-
Cheza chez-
Ona on-
(ii) Mzizi mnyambuliko
Huu ni aina ya mzizi ambao hujengwa na mzizi asilia pamoja na viambishi tamati vijenzi. Mzizi huu mpya hubeba maana ya ziada ya hivyo viambishi.
Kitenzi Mzizi asilia Mnyambuliko Mzizi mnyambuliko
Tema tem Temana Teman
Pata Pat Patisha Patish
Lia Li Lilika Lilik
Kula Kul Liwa Liw
Soma Som Somana Soman
(b) SHINA LA KITENZI
Shina la kitenzi ni mzizi wowote (yaani mzizi asilia au mzizi wa mnyambuliko) uliofunguliwa irabu -a- isiyo na maana maalum ya sarufi.
Mzizi shina
Lim + a lima
Chez + a cheza
Fik +a fika
Liw +a liwa
Vitenzi vyenye asili ya kigeni ambao huishia na irabu e, i, u katika mzizi asilia yao.
Mfano: -
- “arifu”
- “tafiti”
- “samehe”
- “Sali”
- “jibu”
Vitenzi hivyo, mzizi asilia na shina huwa kitu kimoja
Mzizi = shina + a
Shina = mzizi + a
KUBAINISHA MOFIMU AU VIAMBISHI
Kubainisha mofimu (viambishi) ni kitendo cha kutenga neno katika mofimu au viambishi vinavyolijenga.
HATUA MUHIMU KATIKA KUBAINISHA MOFIMU
Hatua zifuatazo ni muhimu katika kubainisha mofimu nazo ni: -
(a) Kutambua aina ya neno ( neno huru au changamano) huundwa na mofimu tegemezi. Neno huru halivunjwivunjwi lakini neno changamano linavunjwavunjwa na kubainisha mofimu zake. Mfano wa neno huru = dada, kaka, mama.
Mfano wa neno changamano = a – na – on – a
= anaona
(b) Kutenga (kuvunjavunja) mofimu au viambishi vinavyounda neno hilo yaani tambua viambishi awali, mzizi, kiini na viambishi tamati. Viambishi na mzizi hupatikana katika neno changamano
Mfano: -
Bainisha mofimu katika maneno yafuatayo na eleza kazi za kila mofimu.
(i) Anasoma - a – na- som – a
1 2 3 4
Kiambishi awali kipatanishi nafsi III umoja
Kiambishi awali cha wakati uliopo
Mzizi wa kitenzi
Kiambishi tamati
(ii) Dunia - hili ni neno huru ambalo huundwa na mofimu hizi hazivunjwivunjwi
(iii) Waliompiga - wa – li- o – m – pig – a
1 2 3 4 5 6
Kiambishi awali kipatanishi nafsi ya tatu wingi
Kiambishi awali cha wakati uliopita
Kiambishi awali rejeshi cha watenda
Kiambishi awali rejeshi cha watendwa
Mzizi wa kitenzi
Kiambishi tamati
DHIMA YA MOFIMU/ VIAMBISHI
Kuonesha nafsi katika kitenzi
Mfano: -
Ni – nasoma= Tu – nasoma - I
U – nasoma = m – nasoma - II
A – nasoma = wa – nasoma- III
Kuonesha njeo katika vitenzi
Mfano: -
A – na – cheza - wakati uliopo
A – li – cheza - wakati uliopita
A – ta – cheza - wakati ujao
Kuonesha umoja na wingi katika nomino na viambishi
Mfano: -
M – toto = wa – toto
Ki – su = vi -su
Kuonesha hali mbalimbali za kitenzi
Mfano: - hali ya masharti
A – ki – ja
A – nge – ku – ja
- Hali ya kuendelea kwa tendo = a – na – li – ma
- Hali timilifu= a – me – sem – a
- Hali ya mazoea= hu - soma
Kuonesha uyakinishi na ukanushi katika vitenzi
Mfano: - ni – nalima - si – limi
A – nacheza - ha – chezi
U – naimba - hu – imbi
Kuonesha urejeshi wa mtenda au mtendwa katika kitenzi
Mfano: - A – na – ye – lima - Mtenda
A – na – u – penda - mtendwa
Kuonesha kauli mbalimbali za vitenzi
Kauli ya kutenda - a – na – pik - a
Kauli ya kutendea - a – na -pik -i – a
Kauli ya kutendewa- a – na – pik – iw – a
Kauli ya kutendeana - wa – na – pik – ian – a
Kauli ya kutendesha - a – na – pik - ish – a
Kauli ya kutendwa - a – na – pik – w – a
TOFAUTI YA MOFIMU NA SILABI
NA
MOFIMU
SILABI
1
Mofimu ni kipashio cha kiima chenye maana kisarufi na kileksia kamusi
Ni sehemu ya neno ambayo huweza kutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu la sauti
Kila mofimu ina kazi maalum kisarufi
(mfano) analima
A – na – lim – a
Si kila silabi ina kazi maalumu mfano silabi ''bali" ikisimama peke yake haiwakilishi maana yoyote kisarufi
Katika mofimu kuna viambishi awali na tamati
Katika silabi hakuna viambishi hivyo
Katika mofimu kuna mizizi, shina la neno
Katika silabi hakuna mzizi wala shina.
Mofimu huru hazivunjwivunjwi, hubaki zilivyo mfano; neno baba lina mofimu huru moja
Silabi huvunjavunja hata mofimu huru mfano;
baba – ba + ba = silabi mbili
Mofimu hazivunjivunji mzizi wa neno mfano;
Lima mzizi lim
Silabi huvunjavunja mzizi wa neno mfano; “analima” lina silabi nne
A - na - li - ma
1 2 3 4
Mara nyingi katika neno kuna idadi ndogo ya mofimu. Mfano; “mama” lina mofimu moja, anacheza lina mofimu nne
Mara nyingi katika neno kuna idadi nyingi za silabi. Mfano;
Mama – lina silabi mbili
Anacheza – lina silabi nne
(c) UUNDAJI WA MANENO KWA KUTUMIA MNYAMBULIKO
Unyambulishaji unatokana na neno “nyambua” ikiwa na maana refusha au vuta kitu.
Mnyambuliko ni kitendo cha uvutaji au urefushaji kipashio / vipashio katika mzizi wa neno. Aidha mnyambuliko unahusu upachikaji wa mofimu zinazofuata mzizi wa neno. Mofimu hizi huitwa mofimu fuatishi (viambishi tamati)
Mfano:-
Soma - Som – e – a
Som – ek –a
Som – esh – a
Som – w – a
Som – ean – a
Som – o
Vitenzi
Vitenzi vyote vya Kiswahili isipokuwa kitenzi kishirikishi “ni” vinaweza kunyambulika.
Mfano: -
Piga – pigia, pigana, pigisha, pigwa, pigiana, cheza, chezea, chezeana, chezeshwa, chezwa.
Baadhi ya majina ya ujumla hupokea viambishi tamati na mengine hupokea viambishi tamati vijenzi.
Mfano: -
Nyumba - nyumbani
Bustani - bustanini
Hewa - hewani
Maji - majini
Viwakilishi
Hivi huchukua viambishi tamati maana
Mfano: -
(a) Viwakilishi vya nafsi kama vile
Mimi - miye
Wewe - weye
Sisi - siye
Ninyi - niye
(b) Viwakilishi virejeshi vya amba.
- Ambalo
- Ambacho
- Ambavyo
Vivumishi
Hivi huchukua viambishi tamati vijenzi
Mfano: -
Safi - safisha, safishwa, safishia, safishika
Fupi - fupika, fupisha, fupishika, fupishwa
Refu - refusha, refushwa, refushika
Viunganishi
Hesabu ndogo ya viunganishi huchukua viambishi tamati vitenzi.
Mfano : - Labda, labdatisha, labdilika, labdishwa.
DHIMA YA MNYAMBULIKO
(i) Mnyambuliko wa maneno hukuza msamiati wa lugha husika.
(ii) Mnyambuliko wa maneno hupanua maana ya maneno.
(iii) Mnyambuliko wa maneno huzalisha kauli mbalimbali za vitenzi kutenda, kutendwa, kutendea, kutendeka, kutendana, kutendeana kutendesha, kutendeshwa.
MATUMIZI YA LUGHA KATIKA MIKTADHA MBALIMBALI
Matumizi ya lugha ni namna ya kutumia lugha, mila, desturi na taratibu za jamii. Ni ambavyo mzungumzaji anatumia lugha yake kuhusiana na msikilizaji.
Hivyo lugha hutegemea
(a) Uhusiano wa wazungumzaji
(b) Mada inayozungumzwa
(c) Mazingira
(d) Dhumuni la mazungumzo
MIKTADHA
Ni mazingira au hali ambamo tukio hutendeka.
Au
Miktadha ni mazingira ya neno katika tungo au sentensi yenye kuzingatia uhusiano wake na maneno mengine.
UMUHIMU WA MATUMIZI YA LUGHA
(i) Kumsaidia mwanafunzi na msomaji wa kawaida kutumia Kiswahili kwa ufasaha.
(ii) Kumsaidia mwanafunzi na msomaji wa kawaida kutofautisha na kutumia mitindo mbalimbali ya Kiswahili
Matumizi ya lugha hutawaliwa na mambo yafuatayo
(i) MAZINGIRA
Msomaji wa lugha yoyote ile anakuwa katika mazingira yanayomtawala kimaisha, mazingira hayo ndiyo yanayomuamulia kuhusu vitendo na hata mazungumzo yake kutokana na mazingira tunapata
- Lugha ya hotelini
- Lugha ya ofisini
- Lugha ya mtaani
- Lugha ya kanisani.
(ii) UHUSIANO BAINA YA WAHUSIKA
Uhusiano baina ya wahusika nao unaathiri uzungumzaji wa lugha hapa mazungumzo au lugha itakayotumiwa itategemea unayeongea naye. Kutokana na uhusiano wa wahusika tunapata
- Lugha ya baba na mama
- Lugha ya watu wa rika moja
- Lugha ya mwalimu na mwanafunzi wa chini yake
- Lugha kati ya mtu na mpenzi wake.
Hapo baba ataongea lugha ya kuamuru na mtoto atajibu kwa unyenyekevu na hivyohivyo kwa mwalimu na mwanafunzi wake, bosi na mfanyakazi wake.
Mfano: -
Lugha ya watu wa rika moja wanazungumza lugha ambayo wenyewe wanaelewa na siyo rahisi mtu wa rika nyingine kuelewa lugha hiyo.
Mfano: -
“Big tunasikia unamic skonga siku hizi”
”Ah si Yule ticha mnoko.... eti kanipakazia ni mchapa daftari wa shule”
“Maticha wetu wanapanga wanipe kibano lakini nikawatoka mie nduki”
“Chekini washkaji, dingi angeniona si ingekuwa so!”
“ngoja niwape siri, nina mishemishe baby ya kuwapa kichapo wale maticha zenu mi nasepa”
“poa mwana”
(iii) MADA YA MAZUNGUMZO
Kimsingi mada ya mazungumzo hutawala usemaji na jinsi ya uzungumzaji kwa ujumla. Kutokana na mada ya mazungumzo tunapata lugha ya
Biashara
Kitaaluma
Mahubiri
Kisiasa
Kisheria n.k
Mfano:
Juma : Nakusikiliza jaribio la kutaka kupindua serikali litakuwa la namna gani katika sheria za Kenya?
Ali : Ni kosa la uhariri
(iv) MADHUMUNI YA MAZUNGUMZO
Hapo mzungumzaji hutoa ufafanuzi wa yale anayotaka kusema
Hivyo ufafanuzi huo utategemea
Mazingira
Uhusiano baina ya wahusika
Mada ya mazungumzo
Mfano: -
Mhadhara/ mazungumzo ya kiuchumi nchini Tanzania yanatofautiana na mhadhara/ mahubiri kanisani.
(v) JINSI YA MAZUNGUMZO
Namna mawasiliano yanavyofanywa kwa maandishi au mazungumzo utaathiri jinsi au mtindo wa uzungumzaji
Mfano: -
Kama mfanyabiashara lazima atapamba uzungumzaji wake kwa kuwavutia wateja
“Mpambe mwanao kwa mia mbili, na mpambe mkeo kwa mia tano”
(A)REJESTA
Ni mtindo wa lugha inayotumika mahali penye shughuli Fulani ambayo ni tofauti na lugha ya kawaida
AINA ZA REJESTA
(i) Lugha ya mitaani/ kijiweni
Haya ni mazungumzo yanayozungumzwa magengeni au katika makundi ya vijana wa rika fulani nayo hueleweka na wazungumzaji wenyewe. Ni lugha ambayo huchipuka kutokana na kikundi cha watu ambacho ni kidogo. Lugha hii hudumu kwa muda mfupi tu halafu hujifia.
Mfano wa maneno yanayosikika mitaani ni kama vile:
- Mshkaji / mtu wangu, mwana wangu besti, (rafiki)
- Demu (msichana)
- Nipe mkwanja( nipe pesa)
- Mzuka (safi, poa)
- Nasepa (naondoka)
- Kitaa (mtaa)
- Skonga (shule)
Kwa ujumla lugha hii siyo sanifu, ni lugha iliyojaa maneno ya mtaani ambayo yanazushwa tu na kundi fulani la wazungumzaji.
(ii) Rejesta ya mahali kwenye shughuli maalumu
Rejesta za namna hii hazifanywi kiholela, bali hufuata taratibu, sheria na kanuni maalum zinazojitokeza katika mazingira haya, mazungumzo ya kwenye shughuli maalumu ni kama vile ya
- Maofisini na mahali popote pa kazi
- Mahakamani
- Hotelini
- Hospitalini
- Kanisani n.k.
Mazungumzo ya hotelini yana utaratibu wake ambao katika mfano
A : Nani wali kuku?
B: Mimi
A: Supu mkia wapi
B : Hapa
Katika mazungumzo hayo “A” anapouliza “nani wali kuku” ana maana kuwa nani anahitaji kula wali na nyama ya kuku. Na wala hakuna maana kuwa mtu anayeitwa.”walikuku “ au “supu mkia”)
(iii) Rejesta zinazohusu watu
Haya mawasiliano yasiyo rasmi huwa ni yale maongezi ya kawaida ya kila siku au mazungumzo rasmi.
Mfano: mazungumzo kati ya
- Vijana wa rika moja
- Wanawake wenyewe
- Mwalimu na mwanafunzi wake
- Wazee wenyewe
- Bosi/ meneja na mfanyakazi wake
(iv) Lugha ya kitarafa
Hiki ni Kiswahili cha tarafa ukikisema katika tarafa nyingine huwa ni vigumu watu wa sehemu hiyo kuelewa anasema nini kwa ujumla ni Kiswahili ambacho kimeathiriwa na vilugha /lugha mama
Mfano:-
Kiswahili cha kiyao- John amenitona (John amenifanya)
Kiswahili cha kiha - Nitakusina (nitakupiga)
Kiswahili cha Kimakonde-Achante chana (asante sana)
Kiswahili cha kihehe - huwaga (huwa)
(v) Kiswahili rasmi/ sanifu
Ni mawasiliano kutokana na vilugha vya lugha ya Kiswahili.
Kiswahili hiki hukubaliwa na wengi katika nchi na ndicho kinachotumika katika shughuli mbalimbali za nchi na vyombo vya habari.
DHIMA (MATUMIZI) YA REJESTA
Rejesta hutumika kama kitambulisho yaani hutofautisha mtindo wa lugha miongoni mwa wazungumzaji kuwa wao ni kundi fulani.
Mfano: -
Rejesta ya watunzi inawatambulisha wao kuwa ni tofauti na ya wavuvi ambao pia wao wana rejesta yao.
Rejesta ya kanisani /msikitini ni tofauti na rejesta ya jeshini n.k
Rejesta hupunguza ukali wa maneno. Rejesta inapotumiwa na kundi la watu huficha jambo hilo linalozungumzwa lisieleweke kwa wengi. Hivyo hadhira inapuuzwa kwa sababu sio watu wengi wanaoelewa.
Rejesta hutumika ili kurahisisha mawasiliano au kupunguza au kuokoa muda wa kuwashughulikia watu au wateja wengi, kwa mfano anayegawa dawa hospitalini anaposema “mbili asubuhi, mchana na jioni) au “kutwa mara tatu” akiwa na maana kwamba mgonjwa anywe vidonge viwili asubuhi, viwili mchana na viwili jioni. Hapa amefupisha ili aweze kuwahudumia kwa muda mfupi wagonjwa wengine wanaosubiri kupewa dawa.
Rejesta hupamba lugha miongoni mwa wazungumzaji kwa mfano rejesta ya hotelini
Mhudumu - nani supu mkia
Mteja - mimi hapa
Mhudumu - wapi wali ng’ombe
Mteja - hapa
Mazungumzo haya kati ya mhudumu na mteja licha ya kuokoa au kurahisisha mawasiliano, vilevile yanapamba mazungumzo haya.
Rejesta huweza kuwa kiungo cha ukuzaji lugha pale lugha inapohusika inapoweza kuunda msamiati wake.
MAMBO YANAYOSABABISHA KUTOKEA KWA REJESTA
UBINAFSI
Yaani tabia aliyonayo mtu ya muda wa kudumu kila mtu ana namna ya kuzungumza ambapo humtofautisha na watu wengine hali hii huleta ubinafsi katika sauti yake (matamshi) na mwisho huleta mtindo wa pekee ambao ni tofauti na wengine.
MWINGILIANO
Makundi ya watu mbalimbali yanapochangamana husababisha mwingiliano miongoni mwao na ili kuweza kutofautisha kundi moja na kundi jingine kuna mambo fulani ambayo hutofautiana miongoni mwa makundi hayo na mambo hayo katika lugha huhusisha matamshi ya maneno, mpangilio wa maneno (sarufi) tofauti hizi husababisha mitindo miwili tofauti miongoni mwa makundi hayo hivyo husababisha kuzuka kwa rejesta.
KUPITA KWA WAKATI
Kila kipindi kwa mitindo yake katika kila mahali. Na hii ni kutokana na mabadiliko ya kihistoria yanayoikumba jamii fulani kila kipindi cha mpito wa kihistoria huweza kuwa na maneno yake ambayo huwa ni tofauti na kipindi kingine cha kihistoria. Vilevile mitindo ya lugha kutoka kipindi kimoja hadi kingine huweza kuwa tofauti. Hivyo rejesta huweza kutoka kati ya kipindi kimoja na kingine.
Mfano: enzi za ukoloni, uhuru, azimio la Arusha, hali ngumu ya maisha n.k
SHUGHULI ILIYOPO
Hapo hutegemeana na mazingira gani ambayo shughuli hiyo inafanyika mfano; msikitini, kanisani, darasani, mahakamani, hotelini, hospitalini, shughuli fulani katika mazingira fulani hutupatia rejesta za mahali.
TOFAUTI ZA HADHI ZA WAHUSIKA (Uhusiano wa wahusika)
Mfano; wasomi au wasiosoma, mwajiri/ mwajiriwa, tajiri/ maskini, hali hii kwa ufupi husababishwa na matabaka yaliyopo katika jamii. Tabaka moja na tabaka jingine hutumia lugha ambayo huwa ni tofauti miongoni mwao hivyo husababisha rejesta kuzuka miongoni mwa matabaka hayo.
MATUMIZI YA UFICHO TAFSIDA
Hali hii pia husababisha kuzuka kwa rejesta kwani husababisha mitindo mbalimbali miongoni mwa wazungumzaji mfano: mwanaume mwenye mambo ya kike huitwa shoga, punga, bwabwa n.k.
(B)MISIMU / SIMO
Misimu/ simo ni maneno yanayosanifu yanayozuka/ zushwa na kikundi cha watu wachache wenye tamaduni moja ili kuelezana mahusiano yao kama kikundi au kuhusu jamii kubwa ambamo vikundi hivyo vinaishi katika kipindi fulani cha muda na hatimaye maneno hayo hupotea na yanayodumu husanifiwa na kuwa msamiati rasmi wa lugha inayohusika.
CHANZO CHA MISIMU
Msimu huzuka kutokana na mabadiliko ya kihistoria yanayoikumba jamii katika nyakati mbalimbali
Misimu mingine huzuka hali ya utani miongoni mwa watu mbalimbali. Mara nyingi misimu ya aina hii hubeba kebehi, dhihaka, bezo, dharau au kusifu kuliko kawaida.
SABABU ZA KUTUMIA MISIMU
Kutaka mazungumzo yawe siri ili yasieleweke kwa watu wengine
Mfano: nafunga ofisi, nasepa
Kudhania ndio ujuzi wa lugha. Hasa kwa vijana walio wengi wakionesha ujana wao. Mfano wanaposema nimewaka au nimechalala ile mbaya au nimefulia.
Kufanya mambo mazito na ya maana kuwa mepesi na ya kawaida mfano mtu anaposema , “kutoa chai” “kula mlungula” – kutoa rushwa/ kula rushwa.
NJIA ZITUMIKAZO KUUNDA MISIMU
(i) Njia ya kufupisha maneno
Neno linaweza kufupishwa makusudi na matokeo yake kuwa ni msimu mfano kwa wanafunzi wa shule za upili katika kidato cha 5 na 6 wana vifupisho vya michepuo yao ya masomo.
Mfano: HKL (Hatusomi Kufaulu Lazima) n.k na chuo kikuu kuna neno DISCO – Mwanafunzi kutoendelea na masomo
(ii) Lugha za kutohoa lugha za kigeni
Kwa kutumia utohozi tunapata misimu kama
Feg - kiingereza “fag” maana sigara
Demu - kiingereza “Dame” maana msichana
(iii) Njia ya kutumia sitiari
Sitiari ni mlinganisho wa ufanano wa umbo, rangi, kimo, dhima/kazi n.k
Baina ya vitu, misimu mingi huundwa kwa njia hii mfano......
(iv) Njia ya kutumia tunakali
Njia hii inatumika pia katika uundaji wa misimu
Maneno kama vile
- Mataputapu - Pombe ya kienyeji
- Malapa (ndala) - Inatokana na sauti inayosikika wakati mtu atembeapo akiwa amevaa kandambili “lap lap”
(v) Njia ya kubadili maana ya msingi
Njia hii nayo imetumika katika uundaji wa misimu mfano mtu kutumia maneno kama vile kumfia, kumzimikia ina maana kumpenda sana.
SIFA ZA MISIMU
Misimu huzuka na kutoweka. Hii ni kutokana na mabadiliko ya kihistoria
Misimu ni lugha isiyo sanifu
Huzushwa na watu kutokana na hisia
Misimu ni lugha ya mafumbo hufahamika na kikundi kidogo cha watu
Misimu ina chumvi/ chuku
Misimu ina maana nyingi
Misimu hupendwa sana na wengi sababu ina mvuto
Misimu huhifadhi historia ya jamii.
AINA ZA MISIMU
Misimu ya pekee
Aina hii ya misimu huelezea mahusiano ya kikundi kimoja kutoka kwenye utamaduni mmoja. Misimu hii hupatikana sehemu moja ya kazi au mahali waishipo watu wa aina moja. Kutokana na jambo hili eneo la matumizi ya misimu ya aina hii huwa ndugu, na kimsingi huibua hisia za aina zote kwa binadamu. Misimu hii huitwa ya kipekee kwa sababu haijulikani nje ya eneo la kuzuka kwake, isipokuwa wale tu ambao wamo katika kikundi hicho, mifano ya watu watumiao misimu ya pekee ni wanafunzi wa shule moja, wafanyakazi wa ofisi ya aina moja, wanamichezo n.k.
Misimu ya kitarafa
Aina hii ya misimu huchukua eneo kubwa au pana kidogo kimatumizi inaweza kupatikana kwenye hata tarafa, wilaya, mkoa n.k watu walioko katika kundi hili wana mchanganyiko wa tamaduni, si rahisi kutambua mipaka ya maeneo haya ya kitarafa, lakini kimsingi yanaweza kuwa ya kijiografia, kihistoria au hata kilugha. Kuenea kwa misimu hii inategemea hali au tabia ya kuingiliana kwa watu katika shughuli za maisha ya siku hadi siku, kama vile biashara, michezo n.k, mara nyingi misimu ya kitarafa hutokana na: -
- Vitu vilivyo katika eneo hili
- Lugha itumikayo katika eneo hili
- Uzoefu wa mazingira na uwezo wa lugha ya msanii.
Misimu zagao
Aina hii ya misimu huenea nchi nzima au hata kuvuka mipaka ya nchi. Misimu zagao hutumika katika mikoa yote na vilevile hutumika katika magazeti, vitabu na vipindi vya redio na television, misimu inayoshika mizizi bila kufutika.
Katika lugha husanifiwa na kuwa msamiati wa lugha
Mfano: - kabwela, wafurukutwa, wakereketwa, buzi, ukapa, wapambe, ngangari, ng’atuka n.k
MATUMIZI (DHIMA) ZA MISIMU
(i) Kukuza lugha
(ii) Kupamba lugha
(iii) Kufanya mawasiliano yawe mafupi na yenye kueleweka kwa haraka.
(iv) Kuwa na siri/ hupunguza ukali wa maneno wakati wa mazungumzo ya kawaida
(v) Kuhifadhi historia ya jamii
(vi) Kuibua hisia mbalimbali za wazungumzaji
(vii) Kufurahisha na kuchekesha
(viii) Kukosoa na kuihasa jamii
(ix) Kuunganisha watu na makundi mbalimbali.
LUGHA YA MAZUNGUMZO NA LUGHA YA MAANDISHI
Maana ya lugha
Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu za binadamu zenye mpangilio maalumu wenye kuleta maana zilizokubalika na jamii husika kwa ajili ya mawasiliano.
Mambo ya msingi yanayojenga maana ya lugha
- Lugha ni sauti za nasibu – kwa sababu mwanadamu hazaliwi na lugha bali huikuta katika jamii.
- Lugha ni sauti zenye maana ambazo mtu huzitoa kupitia ala za sauti kama meno, ulimi,mdomo, kaa kaa n.k
- Lugha ni sauti zenye utaratibu maalumu ambazo hufuata utaratibu fulani uliokubaliwa na jamii ya watu fulani.
- Lugha inatawaliwa na maneno ya utamaduni wa watu fulani kwa kuzingatia mila na desturi za maisha ya watu hao.
- Lugha ni sauti za kusemwa kwa sababu lugha ya asili ya mwanadamu ni lugha ya mazungumzo.
- Lugha ni hali ya binadamu tu, wanyama, ndege na wadudu hawana lugha bali wana milio.
- Lugha ni sauti za kueleza wazi ambazo humwezesha mwanadamu kupashana habari au kujuliana hali na mwenzake.
- Lugha ina maana fulani kwa sababu sauti zinapowekwa kwenye mfumo maalumu ndipo zinapokuwa na maana katika lugha hiyo.
KUNA AINA KUU MBILI ZA LUGHA
(i) Lugha ya mazungumzo na
(ii) Lugha ya maandishi
Lugha ya mazungumzo
Hii ni lugha inayotolewa kwa njia ya mazungumzo ya mdomo.
- Lugha hii hukutanisha pande mbili, mzungumzaji na msikilizaji.
- Lugha hii huonesha hali ya mzungumzaji kama ana hasira, huzuni, furaha.
- Mzungumzaji inabidi aitumie hii lugha fasaha na sarufi na mpango mzuri wa mawazo, uwazi na ukweli katika maelezo yake ili aweze kueleweka kwa msikilizaji wake.
- Msikilizaji nae anatakiwa awe mtulivu na msikivu ili kufahamu yanayozungumzwa aweze kufasiri kupima yale aliyoyasikia kwa uzoefu wake wa siku zote.
SIFA ZA LUGHA YA MAZUNGUMZO
(i) Ina msemaji na msikilizaji. Hii ikiwa na maana kuwa msemaji ndiye chanzo cha mazungumzo na msikilizaji ndiye kikomo.
(ii) Huwakutanisha ana kwa ana msemaji na msikilizaji.
(iii) Hubadilika badilika kutegemeana na mazingira ambayo mtu anaongea pamoja na watu. Hii huibua mitindo mbalimbali ya utumizi wa lugha.
(iv) Huonesha hali ya mzungumzaji mfano, hasira, chuki n.k
(v) Huwasilishwa kuzungumzwa kwa sauti.
(vi) Mzungumzaji hutakiwa azingatie ufasaha na usanifu wa lugha, mpangilio mzuri wa mawazo, uwazi na ukweli katika maelezo yake ili aeleweke.
Lugha ya maandishi
Ni lugha ambayo huwasilishwa kwa njia ya maandishi
- Ni kiwakilishi cha lugha ya mazungumzo
- Lugha hii ni uwezo wa mtu binafsi kutoa mawazo yake na kuyaweka katika maandishi.
- Lugha ya maandishi humlazimu mwandishi atumie muda mrefu kwa sababu huitaji kufikiri kabla ya kuandika pia mwandishi azingatie kanuni na taratibu za uandishi ili kutoa maneno na sentensi sahihi.
SIFA ZA LUGHA YA MAANDISHI
(i) Mwandishi na msomaji, mwandishi chanzo na msomaji kikomo.;
(ii) Nyenzo kubwa ya uwasilishwaji wake ni maandishi.
(iii) Haibadiliki badiliki – ikishaandikwa hubaki vilevile hata kama ni makosa
(iv) Huitaji kufikiri kwa makini kabla ya kutoa. Hivyo ina maadili ambayo mwandishi hufanya ili afanikiwe zoezi lake.
(v) Hudumu kwa muda mrefu kama kumbukumbu baada ya kuandikiwa.
TOFAUTI BAINA YA LUGHA YA KIMAZUNGUMZO NA LUGHA YA KIMAANDISHI
Uwasilishaji
Lugha ya kimazungumzo huwasilishwa kwa njia ya mazungumzo au masimulizi, lakini lugha ya kimaandishi huwailishwa kwa maandishi
Mabadiliko
Mara nyingi sana lugha ya mazungumzo hubadilika kutokana na mazingira, wahusika, mada, wakati na madhumuni yake. Lugha ya kimaandishi haibadiliki pindi tu ikishaandikwa hata kama ilikuwa na makosa.
Uhusiano na hadhira
Lugha ya mazungumzo huwakutanisha ana kwa ana, mzungumzaji na msikilizaji, lakini lugha ya kimaandishi haiwakutanishi ana kwa ana mwandishi na msomaji.
Maandalizi
Lugha ya mazungumzo haihitaji maandalizi makubwa ya mada, lakini lugha ya maandishi ili kutafakari mambo yatakayoandikwa na huandaa vifaa kama vile peni, rula, karatasi n.k
Uhifadhi
Lugha ya kimazungumzo huhifadhiwa kwa kichwa hivyo si rahisi kukumbukwa kwa muda mrefu, lakini lugha ya kimaandishi huhifadhiwa kwenye vitabu na majarida ambapo hudumu kwa muda mrefu.
Gharama
Lugha ya kimazungumzo haihitaji gharama nje ya ala za sauti ili kuwezesha kutamka maneno vizuri.
Lugha ya kimaandishi ina gharama kubwa kwa sababu huhitaji vifaa vya kuandikia kama karatasi, kalamu na vifaa vingine ili iandikwe kwa ukamilifu na muda.
Wahusika
Lugha ya mazungumzo ina utajiri wa wahusika. Ni lugha ya kila mtu ajifunzayo toka utotoni, hivyo wazungumzaji ni wengi.
Lugha ya kimaandishi wahusika ni wachache kwani ni wale tu wawezao kusoma na kuandika.
Uhai
Lugha ya kimazunguzo ina uhai kwani kuonesha ujumbe pamoja nakuelezea hali ya mzungumzaji kama ana hasira, chuki, furaha n.k
Lugha ya kimaandishi ni vigumu kuonesha na kuelewa wazi hali ya mwandishi.
DHIMA YA LUGHA YA KIMAZUNGUMZO NA YA KIMAANDISHI
(DHIMA YA LUGHA KIUJUMLA)
- Lugha ni chombo cha lazima na muhimu katika mawasiliano ya binadamu yaani hutumika katika kupashana habari.
- Lugha ni chombo muhumu katika kufundishia elimu kuanzia ngazi za chini hadi ya juu.
- Lugha ni chombo muhimu katika kuleta maendeleo kwa sababu hutumika katika kuhimiza shughuli za maendeleo ya jamii.
- Lugha ni alama ya utambulisho ambayo hutumika kutambulisha jamii juu ya taarifa fulani, watu fulani au kabila fulani.
- Lugha ni chombo muhimu katika kuleta maelewano na upatanisho miongoni mwa wanajamii.
- Lugha ni chombo muhimu katika kutunza kumbukumbu za jamii husika.
MAKOSA YA KISARUFI NA KIMANTIKI
Lugha inapotumika vibaya hupoteza lengo na madhumuni ya mzungumzaji kwa msikilizaji wake. Upotoshaji huu unaweza kujitosheleza katika sarufi au mantiki.
Makosa ya kisarufi
Makosa ya kisarufi hujumuisha makosa ya kimsamiati, kimuundo, kimaana na kimatamshi. Vipengele hivi vikitumiwa vibaya basi makosa hayo ni msamiati.
Miundo ya sentensi, upatanisho wa kisarufi na matamshi
(a) Kosa la msamiati
Baadhi ya watu huchanganya msamiati wakati wa kuzungumza. Hali hii husababisha kosa la kimsamiati mfano mtu huchanganya neno mazingira na mazingara kwa kudhani maneno yote yana maana sawa.
(b) Kosa la miundo ya sentensi
Vilevile makosa ya miundo ya sentensi hujitokeza kwa sababu ya kukiuka miundo ya sentensi ya Kiswahili.
Mfano:
Mtu akisema Simba aliuwawa na mwindaji, hapa msikilizaji anaweza akapata maana mbili.
(i) Msikilizaji anaweza kuelewa mwindaji alimwua simba au simba pamoja na mwindaji walikufa wote.
(ii) Nilimpikia uji bibi.
Maana – Alifanya tendo la kupika uji kwa ajili ya bibi
Alipika uji badala ya bibi
(c) Kosa la upatanisho wa kisarufi
Makosa ya upatanisho wa kisarufi pia huathiri sana lugha kati ya mzungumzaji na msikilizaji, kwa kawaida katika Kiswahili nomino mtenda ndiyo inayotawala upatanisho wa kisarufi kwenye kivumishi na kitenzi mfano mtu anaweza kukosea na kutamka
(i) Mtoto mdogo analia
Watoto wadogo wanalia
Mtoto wanacheza mpira
Mtoto anacheza mpira
(d) Kosa la kimatamshi
Makosa ya kimatamshi nayo ni sehemu ya makosa ya kisarufi watu wengine hushindwa kutamka baadhi ya maneno (sauti) ya lugha ya kishwahili sanifu.
(a) Kura na kurara je? - Kula na kulala je?
(b) Msichana mhodari - Msichana hodari
(c) Selasini na thaba - Thelathini na saba
(d) Achante sana - Ahsante sana
(e) Ng’ombe wako ngambo ya mto
- Ng’ombe wako ng’ambo ya mto
Makosa ya kimantiki
Mantiki ni mtiririko wa fikra zilizopangwa ili kujenga hoja yenye kukubalika. Kosa la kimarufuku ni hali ya kukosa utaratibu mzuri wa kufikiri hasa wakati wa kuzungumza na kuandikwa
Mara nyingi tatizo hili hutokea kwa sababu ya upotofu wa mawazo ya mzungumzaji.
Mfano:
(a) Nyumba imeingia nyoka
Nyoka ameingia kwenye nyumba
(b) Jicho limeingia mdudu
Mdudu ameingia jichoni
(c) Chai imeingia nzi
Nzi ameingia kwenye chai
(d) Mfupa hauna ulimi
Ulimi hauna mfupa
- Kusahihisha makosa
Makosa ya kawaida yataendelea kuwepo katika lugha yoyote ile kama vile Kiswahili kwa hiyo hatuna budi kujitahidi kuzuia makosa hayo.
Inatubidi kuhakikisha makosa ya kisarufi na kimantiki katika msamiati, matamshi, muundo na maana hayajitokezi kwenye mazungumzo, barua, shuleni na kwenye vyombo vya habari kama vile redio, televisheni na magazeti
Vilevile jitihada za marekebisho ya kisarufi na kimantiki sharti zitiliwe maanani tangu kiwango cha elimu ya msingi, sekondari na vyuoni hadi vyuo vikuu.
Mara nyingi makosa ya kimsamiati husababishwa na vyombo vya habari kwa hiyo ni muhimu somo la utumizi wa lugha ya Kiswahili lizingatiwe sana katika vyombo vya habari ili kuepusha upotoshaji wa jamii.
Kwahiyo kamusi ni kitabu muhimu sana kwa sababu huwa na orodha ya maneno tofauti yanayotumiwa na wazungumzaji na maana zake.
-Makosa ya kisarufi
Ni ukiukaji wa kanuni, sheria na taratibu za lugha kimatamshi, kimsamiati kimuundo na kimaana.
-Makosa ya kimantiki
Ni hali ya kukosa utaratibu mzuri wa kufikiri hasa wakati wa kuzungumza au kuandika
Kufanana kwa lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi
(a) Lugha zote hutumika katika kufanya mawasiliano na kupashana habari.
(b) Lugha zote ni mali ya mwanadamu mwenyewe
(c) Lugha zote huwa na mada inayozungumziwa au kuandikwa ili kueleweka vizuri kwa msikilizaji au msomaji inabidi kuwe na mpangilio mzuri wa mada na mtiririko mzuri wa mawazo.
(d) Lugha zote zina chanzo na kikomo, chanzo cha lugha ya maandishi ni mwandishi na lugha ya mazungumzo ni mzungumzaji na kikomo ni msomaji na msikilizaji.
(e) Vilevile lugha zote hutumika katika kuhimiza shughuli zote za maendeleo ya jamii kwa sababu huleta maendeleo, amani na mshikamano kwa jamii husika.
Matamshi na lafudhi ya Kiswahili
Lugha ya Kiswahili na mfumo wake wa matamshi. Matamshi na lafudhi ya Kiswahili imeathiriwa sana na lugha nyingine za kibantu kwa watanzania wengi, Kiswahili ni lugha ya pili, lugha ya kwanza ni ya makabila kama vile:
Kisukuma, kinyamwezi, kiluguru, kiha, kichaga, kihaya n.k
Kiswahili kina lafudhi yake ya matamshi sahihi ya kutamka , mara nyingi huathiriwa na lugha mama
Lafudhi
- Ni matamshi ya mzungumzaji yanayotokana na lugha yake (lugha mama) ya mwanzo au lugha ya zinazozunguka.
Matamshi
- Ni kitendo cha kutoa nje ya kinywa au pua ya mwanadamu sauti ambazo hutumika katika mazungumzo au usemi wowote.
Kosa sahihi
Ch sh
Chabiki shabiki
Changa shanga
Mchenga mshenga
-g- -gh-
Garama gharama
Magaribi magharibi
Buguza bughuza
-f- -v-
Futa vuta
Fita vita
Faa vaa
-L- -r-
Lika rika
Fahali fahari
Hawala hawara
-ng- ng’
Ngombe Ng’ombe
Ngara Ng’ara
Mngao Mng’ao
Nt nd
Ntani ndani
Ntungu ndugu
Ky ch
Kyai chai
Kyama chama
K g
Kari gari
Kama gama
S z
Saa zaa
Kasa kaza
Z j
Zana jana
Zua jua
Z au s th
Zamani thamani
Selasini thelathini
Matamshi na lafudhi ya Kiswahili huweza kuathiri hata sentensi ya Kiswahili mfano sentensi hizi hazina lafudhi na matamshi sahihi ya Kiswahili.
(a) Kyai kya moto kimeletwa na mpishi
Chai ya moto imeletwa na mpishi
(b) Ngombe watarejea zizini magaribi
Ng’ombe watarejea zizini magharibi
(c) Kuathiriwa kwa lafudhi na matamshi sahihi ya Kiswahili huweza kutokana na
(a) Athari za lugha mama. Mfano mpare hutumia th badala ya s
Thatha - sasa
Thithi - sisi
Thote - sote
Mfano: Thithi thote tunywe thupu
Sisi sote tunywe supu
(b) Mzungumzaji kuwa na kithembe
Mfano:
Thamba - shamba
Dithemba - disemba
Thema - sema
(c) Maumbile / ukosefu wa ala fulani za sauti
- Mtu asiye na meno hushindwa kusema ala zinazotamkwa kwenye meno mfano:
Dhahabu - zahabu
Dhambi - zambi
(d) Kutumia neno bila kuzingatia mazingira au muktadha unaohusika na utumizi wa maneno hayo
UTATA KATIKA MAWASILIANO
Mawasiliano ni mchakato wa upashaji na ubadilishaji wa habari kwa njia mbalimbali.
Mara nyingi utata wa lugha ya Kiswahili huweza kujitokeza katika tungo neno au tungo sentensi.
Sababu za utata
(a) Uwezo wa neno moja kuwa na maana zaidi ya moja mfano mbuzi.
(b) Kutozingatia taratibu za uandishi
Mfano:
Tulimkuta Juma na rafiki yake, Abdi
Tulimkuta Juma na rafiki yake Abdi
Sentensi ya (1) ina maana kuwa tuliwakuta watu wawili yaani Juma na rafiki wa Juma aitwaye Abdi (mkato maana yake)=
Sentensi ya (2) ina maana kuwa tulimkuta juma na mtu mwingine ambaye ni rafiki wa abdi
(c) Kutumia maneno yenye maana ya picha au maana iliyofichika mfano ‘ua’ lina maana ya
- Wigo
- Sehemu ya maana
- Binti mzuri, hii ni lugha ya picha
(d) Kutotamka neno ulilokusudia kwa usahihi mfano: zana – dhana
Utata uliojitokeza katika maneno na katika sentensi
UHAKIKI WA KAZI ZA KIFASIHI SIMULIZI
Fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na watumiaji wake.
Fasihi simulizi ndiyo fasihi ya awali, fasihi simulizi imeanza wakati binadamu alipoanza kutumia lugha kama chombo cha mawasiliano ndipo alipoanza kutumia methali, nyimbo, vitendawili n.k. Fasihi simulizi hurithiwa kutoka kizazi kimoja na kingine.
Fasihi simulizi huundwa sambamba na mabadiliko ya jamii kwa hiyo nayo hubadilika kifani na kimaudhui ikifuata mabadiliko ya mifumo ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.
Kwa maana hiyo basi fasihi simulizi ni fasihi iliyo hai na hubadilika kulingana na mahitaji ya jamii.
Vipengele vya fasihi simulizi
(a) Msimuliaji (fanani)
Huyu ni mtu anayeitamba hadithi, kitendawili au nahau.
(b) Hadhira
Hawa ndio wanashiriki kama wasikilizaji na fanani huwatumia kama wahusika na fani zake.
(c) Tukio
Ni tendo linalofanyika katika jukwaa la fasihi simulizi. Tendo linaweza kuwa, kuimba, kutega vitendawili au kutamba hadithi.
(d) Utendaji Ni tendo linalofanyika katika jukwaa la fasihi.
(e) Uwanja wa kutendea
Ni mahali ambapo tukio la fasihi simulizi linafanyika, inaweza kuwa uwanjani, baharini n.k
Tanzu nne za fasihi
(a) Hadithi - ngano, visakale,visasili na vigano
(b) Ushairi - Ngonjera ,tenzi , shairi, nyimbo
(c) Semi - nahau, mafumbo, vitendawili, methali
(d) Sanaa ya maonyesho (maigizo), vichekesho, majigambo
UHAKIKI
Nini maana ya uhakiki wa fasihi simulizi?
Ni kazi au kitendo cha kuchambua na kufafanua kazi za fasihi simulizi ili kuweza kupata maadili na ujumbe wa kazi hiyo.
Mhakiki
Ni mtu anayejishughulisha na uhakiki wa kazi za fasihi zilizotungwa na wasanii wengine.
VIGEZO VYA UHAKIKI
(i) UKWELI WA MAMBO
Mhakiki wa kazi za fasihi atajiuliza, je ni kweli kuwa jambo hilo linafanyika katika jamii inayozungumzwa.
Mfano:
Kama Mhakiki wa fasihi simulizi anahakiki ngonjera inayohusu rushwa inabidi ajiulize je kweli kuna rushwa katika jamii inayomzunguka.
(ii)Uhalisi wa mambo
Mhakiki wa kazi za fasihi atalingalisha wahusika, mazingira na matukio katika kazi hiyo ya fasihi simulizi na hali halisi.
Je yanayotendeka kwenye kazi ya fasihi simulizi yapo katika jamii yetu. Mfano: kama hadithi inahusu uchoyo, mhakiki inabidi ajiulize. Je katika jamii husika tabia ya uchoyo ipo.
(iii) Umuhimu wa kazi za fasihi simulizi
Mhakiki ataangalia jambo ambalo linazungumziwa kwenye hiyo kazi ya fasihi simulizi kama ina umuhimu na kuelimisha katika jamii. Jambo linalozungumziwa linaweza kuwa la kweli lakini halina umuhimu kwa jamii hiyo.
Mhakiki wa kazi za fasihi huzingatia vipengele vikuu viwili vya kazi navyo ni: -
Fani
Ni umbo la nje la kazi ya fasihi ambalo vipengele vyake ni matumizi ya lugha, mtindo, muundo, mandhari na wahusika.
Maudhui
Ni umbo la ndani la kazi ya fasihi ambalo pia hujumuisha dhamira, ujumbe, mafunzo, migogoro na falsafa
Kwa hivyo vipengele na vigezo vya uhakiki ndio kipimo cha ubora na udhaifu wa kazi ya fasihi simulizi katika tanzu na vipera vyake.
UHAKIKI WA USHAIRI WA FASIHI SIMULIZI
Ushairi katika fasihi simulizi ni fungu linalojumuisha tungo zote zenye kutumia mapigo kwa utaratibu maalumu, mathalani mapigo hayo yanaweza kupangwa kwa muwala wa urari wa vina na mizani. Baadhi ya fani za ushairi huambatana na muziki wa ala na wakati mwingine hupata mizani yake kutokana na mipangilio ya ala.
Vipengele vya fani katika ushairi
(i) Muundo
Mashairi yana miundo mbalimbali kutegemeana na ufundi wa mshairi mwenyewe. Katika muundo tunaangalia kile kinachoonekana kwa nje mfano:
- Mgawo wa vipande
- Idadi ya mistari katika kila ubeti
- Kiitikio / mkarara/ kibwagizo
- Idadi ya beti katika shairi zima
Kwahiyo katika mashairi tuna miundo mbalimbali ambayo hutumiwa kuainisha kwa mujibu wa idadi ya mistari katika kila ubeti muundo huu ndio hutupa mashairi ya tathnia (mistari 2) tathlitha (mistari 3) Tarbia (mistari 4) Takhmisa (mistari 5) n.k
(ii) Mtindo
- Mashairi ya fasihi simulizi yana mitindo mingi sana katika utungaji wake
- Mtindo tunaangalia vipengele kama vile:
Urari wa vina na ulinganifu wa mizani (ushairi unaozingatia sheria za urari wa vina na mizani ni mashairi ya kimapokeo).
- Mizani – ni idadi ya silabi ambazo zipo katika kila mstari
- Vina – ni silabi zenye mlio unaofanana
- Mtindo wa pindu ambapo silabi mbili za mwisho wa mstari hurudiwa rudiwa, mfano kama mstari wa kwanza huishia na neno “fahamu” basi mstari wa pili pia utaishia na silabi “mu”
Mashairi ya masivina (gum / mauve)
Haya ni mashairi yasiyofuata urari wa vina na mizani
(iii) Hisia
Katika hisia tunajiuliza maswali yafuatayo
Ni hisia gani zinazowasilishwa na ushairi huo, mfano za huzuni, furaha kukatisha tamaa, kuchekesha, kuudhi, kuogopesha au ujasiri. Kwa kawaida mshairi aandikapo shairi huanza yeye mwenyewe kukumbwa na hisia fulani ambazo hujaribu kuzitoa kwa njia ya ushairi ili ziwasilishwe kwa hadhira yake.
(iv) Utendaji
Hapa tunaangalia vipengele kama vile mtindo na utendaji. Unatendwa na watu wengi au mtu mmoja, moja kwa moja ama mtu akijibizana na kundi la watu wengi kwa zamu.
Pia inabidi kuzingatia mbinu za utendaji, kama vile malighati ukariri au majibizano (ngonjera) na uimbaji.
Muktadha (mazingira)
- Ushairi unaimbwa wapi? Wakati gani na kwa hadhira ya aina gani? Watendaji akina nani, wazee,vijana, wanawake/ wanaume
(v) Wahusika
Vilevile ushairi wa fasihi simulizi huwa na wahusika, fanani na hadhira.
- Fanani ndio huwa wanatumiwa na mtunzi kufikisha ujumbe kwa hadhira.
- Fanani anaweza kuwa muimbaji, waghanaji n.k
- Vilevile tanzu za fasihi simulizi hutumia hadhira kama waitikiaji. Jukumu kubwa la waitikiaji ni kumpumzisha fanani hasa mwimbaji.
- Kwa upande wa ngonjera kunakuwa na wahusika pande mbili ambapo kunakuwa na malumbano kati yao. Madhumuni yao ni kutoa ujumbe fulani mhusika mmoja anaweza kusema jambo moja kutoka ubeti na mwingine kulijibu.
(vi) Matumizi ya lugha
- Lugha ndio malighafi ya ushairi. Lugha inayotumika ni ile inayokusudiwa kuinua hisia fulani kwa hadhira yake.
- Matumizi ya lugha katika ushairi kuna ya aina mbalimbali. Uteuzi wa maneno (msamiati) lazima uzingatie kile unachozungumzia.
- Uteuzi wa maneno/ msamiati – mambo ya kuzingatia hapa kuhusiana na msamiati na ushairi ni: -
- Matumizi ya maneno ya kale ili kuleta ulinganifu wa vina na mizani. - Kuendeleza msamiati ili kuleta uhusiano wa vipindi mbalimbali vya kihistoria na pia kukejeli jambo au hali fulani.
- Matumizi ya maneno yaliyobuniwa na msanii mwenyewe
- Matumizi ya maneno ya kawaida yenye muundo usiokuwa wa kawaida.
- Matumizi ya tamathali za semi
Kuna aina mbalimbali za semi
Sitiari
Ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili pasipo kutumia viunganishi. Mfano, mfalme ni simba
Tashihisi (uhuhishi)
Ni mbinu ambayo kitu ambacho hakina uhai kinapewa uwezo wa kutenda kama binadamu.
Tashbiha
Ni kufananisha kitu au jambo kwa kutumia maneno kama mithili ya, kama, mfano ( au viunganishi)
Takriri
Ni marudiorudio ya maneno, silabi, sentensi hii ni katika kusisitiza maudhui na kupamba lugha.
Kejeli (kinayo)
Ni kumpa mtu sifa asiyofanana nayo. Mbinu nyingine za kisanaa.
Taswira
Ni maelezo ambayo yanatumika kuunda/ kuchora picha ya kitu, hali, wazo au dhana fulani akilini mwa msomaji/ msikilizaji.
Ni dhana au wazo ambalo msanii anatumia katika kazi yake ya fasihi ili kuwakilisha wazo, dhana ya kitu kingine
Mfano; Ua – inaashiria mpenzi/ mwanamke mzuri
Tafsida
Ni kutumia lugha iliyo fasili siyo kali ili kuficha maneno machafu au yanayokarahisha yasitumike.
Vilevile msanii hutumia misemo na nahau- hii ni katika kuipamba kazi yake ya fasihi simulizi na pia katika kutajirisha maelezo yake.
Matumizi ya methali
Pia msanii hutumia methali katika ushairi ili kupitishia hekima vilevile zinatumiwa ili kujenga kejeli kuhusu masuala mbalimbali ya jamii.
UHAKIKI WA MAUDHUI YA USHAIRI WA FASIHI SIMULIZI
Vipengele vya maudhui katika ushairi wa fasihi simulizi
Maudhui: - Ni jumla ya mawazo yote yanayozungumziwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Maudhui hujumuisha mawazo pamoja na mafunzo mbalimbali yanayomsukuma msanii hadi akatunga kazi fulani ya fasihi.
DHAMIRA
- Ni kiini cha suala linalozungumziwa na msanii katika kazi ya fasihi. Katika ushairi huwa kuna dhamira kuu ambayo huwa ni kiini cha kazi ya msanii na dhamira ndogondogo ambazo zinaundwa sambamba na dhamira kuu.
- Wasanii wa ushairi wameshughulikia dhamira tofauti tofauti kama vile: -
Mapenzi na ndoa, migongano ya kitabaka, mwanamke na nafasi yake katika jamii, maadili mbalimbali ya jamii, ukombozi, ujenzi wa jamii mpya n.k
UJUMBE NA MAADILI
- Ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma au kusikiliza ushairi wa fasihi simulizi.
FALSAFA
- Ni jinsi ambavyo msanii anaweza kulinganisha mambo kisanaa akihusisha na maisha.
- Ni mwelekeo wa imani ya msanii
MSIMAMO
- Hii ni hali ya msanii kuamua kushikilia jambo fulani. Jambo hilo linaweza likawa halikubaliki lakini akalishikilia tu.
UHAKIKI WA MAIGIZO
Maigizo
- Ni sanaa ambayo huwasilishwa ana kwa ana, tukio fulani kwa hadhira kwa kutumia usanii wa kiutendaji
- Maigizo huliweka wazo katika hali ambayo linaweza kutendeka kwa kutumia usanii wa utendaji kama vile vitendo, uchekeshaji, ngonjera n.k
- Maigizo ni mpangilio wa maneno ambayo huambatana na utendaji wa wahusika. Wahusika huwa wanaiga mambo yanayopatikana na jinsi yanavyoonekana kwa jamii. Lugha ya wahusika inaingiliana kwa kiasi kikubwa na lugha ya jamii inayohusika. Hii ni lugha ambayo pia inatumia picha, mafumbo, tamathali za semi na ina ubunifu wa kuvutia hadhira.
- Uigizaji ni muhimu katika fasihi simulizi. Katika uigizaji huu, watendaji huiga tabia na matendo ya watu au viumbe wengine katika kutoa ujumbe fulani. Uigizaji huu unaweza kuwa na nia ya kukejeli, kudhihaki, kukosoa au hata kuburudisha
Vipera vya maigizo
(a) Michezo ya jukwaani
- Ni mpangilio wa mazungumzo baina ya watu unaoambatana na utendaji wao. Mazungumzo hata hujenga kisa chenye mgogoro au migogoro ya jamii.
- Mgogoro unaweza kuwa vita baina ya serikali na wauza madawa ya kulevya, demokrasia dhidi ya udiktekta,ukale na usasa, uonevu dhidi ya haki na kadhalika.
- Michezo ya kuigiza huonesha mambo ambayo yalitokea, yanayotokea au yanayotarajia kutokea.
- Mhusika wa mchezo anaweza kuigiza kazi mbalimbali kama vile kulima, kutibu watu, kufundisha darasani, kuuza vitu dukani n.k
- Mfano wa muundo wa mchezo wa jukwaani (kuigiza)
MUNGU - Rosa kwanini umejiua
ROSA - Ee Mungu wangu! Haya yote yametokea kwa sababu ya babu yangu
MUNGU - Rosa nakuuliza tena, kwanini umejiua?
ROSA - Ee Mungu wangu! Haya yote yametokea kwa sababu ya babu yangu
MUNGU - Zacharia una usemi gani wa kujitetea?
ZACHARIA - Ee Mungu wangu! Haya yote yametokea kwa sababu ya ubaya na udhaifu wake mwenyewe.
MUNGU - Rosa unauhakika?
ROSA - Ndio bwana!
(b) Vichekesho
- Ni aina ya maigizo ambayo ni mafupi yenye lengo kuu la kufikisha ujumbe kwa njia ya kuburudisha na kuchekesha hadhira.
- Vichekesho vimeundwa na mpangilio wa maneno ulio na utendaji ambao hauna uchambuzi wa undani kuhusu kisa kinachooneshwa na pia wakati mwingine, vichekesho hutendwa kwa lengo la kuchekesha na kupitisha wakati
Mfano:Mizengwe,komedi
(c) Majigambo
- Ni maigizo yenye kujigamba kwa mtu aliyefanya mambo ya maana au kishujaa yasiyo ya kawaida
Mfano: -
Kuua simba, kumdhuru adui.
- Mara nyingi majigambo hutungwa na kughaniwa na mhusika mwenyewe ambaye hutumia misemo na tamathali za semi mbalimbali.
- Fanani ya majigambo hutumia lugha ya mficho ambayo imesheheni matumizi ya taswira na ishara mbalimbali.
(d) Ngonjera
- Ni mpangilio wa beti au mashairi ya kujibizana unaoambatana na utendaji. Kila mhusika anatoa ubeti wake huku akitenda vitendo vinavyolingana na asemacho.
- Muundo wa ngonjera ni wa shairi na unatendeka
- Ngonjera huigizwa hadharani kwa lengo la kuzungumzia mambo au mawazo mazito ya kijamii au kibinafsi.
- Kigezo cha kufanya vitendo wakati wa masimulizi ya ngonjera ndicho kinachosababisha ngonjera kuwa mojawapo ya kipera katika utunzi wa maigizo.
(a) FANI
- Uhakiki wa fani ya maigizo unaangalia vipengele vifuatavyo Tendo / Tukio
Katika maigizo lazima pawe na tukio ambalo huchukuliwa kama kiini au chanzo cha utunzi huu.
Tendo au tukio, huwa ndio kishawishi cha fanani wa maigizo, kwa hiyo katika maigizo lazima pawe na tendo linalotendeka, yaani tendo linalo lidhihirisha katika umbo la vitendo vikitendwa.
(b) WAHUSIKA
- Katika maigizo kuna wahusika wa aina mbili
(i) Watendaji
(ii) Watazamaji (hadhira)
Watendaji
- Ni wasanii ambao hutumia vipawa vyao kwa lengo la kuonesha dhana fulani kwa hadhira.
- Hawa hutumia mbinu mbalimbali kwa lengo la kuvutia hisia kwa hadhira zao hasa kwa kutumia viungo vya mwili
- Katika maigizo kuna watendaji wakuu na wadogo.
- Watendaji wakuu ndio wanaobeba kiini cha dhamira kuu na maana ya igizo lenyewe pia huonekana kuanzia mwanzo wa onesho hadi mwisho. Matendo yote hujengwa kumhusu yeye.
- Watendaji wadogo hawa hujitokeza hapa na pale katika onesho fulani ili kukamilisha onesho hilo.
Hawa husaidia kujenga dhamira fulani katika igizo vilevile husaidia katika kumjenga mtendaji mkuu.
Watazamaji (hadhira)
- Watazamaji katika muktadha huu inamaana watu walio kusanyika kwa makusudi ya kutazama igizo lolote lile.
- Watazamaji huhisi, husikia, hutafakari ili waweze kutoa uhakiki wa vipengele mbalimbali vya igizo hilo
- Hadhira huwa na uhuru wa kudadisi na pia kushiriki kwa kucheza kuimba na kupiga vigelegele.
- Hadhira ndio huwa wahakiki wa kwanza wa igizo lolote lile. Hadhira huakiki igizo la mtendaji kwa vile vitendo, mwenendo na vitabia anavyofanya mtendaji katika jukwaa vina ukaribu mkubwa sana kwa kila siku
Mandhari (Uwanja wa kutendea)
- Mandhari inamaana ya mahali popote ambapo watendaji hutumia kuonesha onesho hilo.
- Mandhari inaweza kuwa uwanjani, barabarani, nyumbani, porini au jukwaani.
- Katika jukwaa hili mtendaji, huwa na uhuru wa kutenda kuingia na kutoka jukwaani bila wasiwasi.
- Zamani michezo mingi iliigizwa nje na waigizaji hawa huangalia sana umuhimu wa jukwaa kwani jukwaa ilikuwa sehemu yoyote ile, kama ni darasani, uwanjani n.k
- Siku hizi wale ambao wanasoma shule za upili wana utaratibu mzuri wa kutumia jukwaa kwa maonesho hufanya hivyo kiasi kwamba kama jukwaa halina pazia wanaona shida kuigiza katika jukwaa hilo.
Muundo
- Muundo katika maigizo tunaangalia mpangilio wake yaani umbo lake lilivyogawanyika kwenye sura au maonyesho au mtiririko wa matukio na msuko.
- Matukio yanaweza kufanana moja kwa moja au yakawa na uchangamano ambao huusisha kwenda mbele na kurudi nyuma (msuko changamani)
Mtindo
- Maigizo hutumia mtindo wa dayolojia yaani majibizano kati ya wahusika waliopo kwenye jukwaa. Hata hivyo kutambua ni muhimu kuwa mazungumzo hayo siyo maongezi au majibizano kwa ajili ya kujibizana tu mazungumzo lazima yaendane na tendo kuu katika maigizo. Mazungumzo ndiyo nguzo ya kukidhi maudhui na dhamira.
Matumizi ya Lugha.
- Lugha ndiyo nyenzo kuu ya maigizo. Dhamira na maudhui hayawezi kuwakilishwa na kuwafikia watazamaji bila kuwako lugha.
- Uchunguzi na matumizi ya lugha ni muhimu katika uhakiki wa maigizo.
(a) Matumizi ya methali
Katika maigizo methali hutumika ili kupitisha hekima, kujenga kejeli kuhusu masuala mbalimbali ya jamii, kujenga mandhari ya kiutamaduni ya kuaminika kuhusu jamii.
(b) Misemo na nahau
- Matumizi ya misemo na nahau katika kazi za fasihi hushabihiana sana na yale ya methali.
- Misemo na nahau hutumika kutambulisha mazingira maalum au kujulisha hadhira wakati na wahusika katika kazi ya fasihi inayoshughulikiwa.
- Hii ni kwasababu msemo huzuka na kutoweka kutokana na hali mbalimbali za kimazingira.
- Misemo, misimu, nahau huzaliwa hukua na hata kufa kwahiyo basi matumizi yake katika kazi ya fasihi nayo hutegemea uhai wa misemo, nahau na misimu.
- Vilevile misimu na nahau hutumiwa kwa njia ya kupamba kazi ya fasihi na pia katika kuainisha wahusika na lugha zao. Vilevile hutumiwa na wasanii kutayarisha maelezo yao.
(c) Tamathali za semi.
Hizi ni nahau, maneno au sentensi ambazo hutumiwa na wasanii wa fasihi ili kutia nguvu katika maana, mtindo na hata sauti katika maandishi ama kusoma. Na wakati mwingine tamathali za semi hutumiwa kwa ajili ya kuipamba kazi ya fasihi pamoja kuongeza utamu wa lugha.
Kuna aina nyingi za tamathali za semi kama vile
(i) Tafsida
- Hii ni kupunguza ukali wa maneno au matusi katika usemi.
Mfano kujisaidia au kuenda haja badala la kunya/ kukojoa.
(ii) Kejeli /stihizai
- Hii kazi yake ni kuleta maana iliyo kinyume na ile iliyokusudiwa ama kinyume na ukweli ulivyo. Lengo lake ni kutaka kuzuia matatizo ya mgongano pindi itumikapo kwa lengo maalumu la kufundisha au kuasa.
Mfano:
-Mtu mchafu lakini anaambiwa
“sijaona mtu msafi kama wewe”
-Mtu ni adui
“wewe ni rafiki kipenzi”
(iii) Dhihaka
- Hii ni tamathali ya dharau na ina lengo la kumweka mtu katika hali duni kupita kiasi lakini kwa mbinu ya mafumbo.
Mfano:
“Adella alikuwa msichana msafi sana ndio maana kila mara alipaka mafuta yaliyonukia na kusababisha nzi walioleta matatizo makubwa”
(iii) Sitiari
- Ni tamathali inayolinganisha matendo au tabia vitu vyenye tofauti bila viunganishi
Mfano:
o Bwana Salumu ni mkaa kabisa
o Penzi ni maua/ upepo/ kikohozi
o Maisha ni moshi
o Shani ni shamba
o Uchoyo ni sumu
(iv) Tashbiha
Tamathali inayolinganisha vitu kwa kutumia viunganishi kama vile, kama, mfano wa, mithili ya, kana kwamba, sawa na n.k
Mfano:
John ni mweusi kama mkaa
Ana sauti tamu sawa na chiriku
(v) Tashihisi
- Vitu visivyo na sifa kama walizonazo wanadamu, kupewa sifa za kutenda kama binadamu
Mfano mawimbi ya bahari yaliimba wimbo wa mahaba huku upepo mwanana ukiwanong’oneza siri ya mapenzi. Wapenzi wale wawili waliokuwa wamekumbatiana chini ya kivuli cha mti
Mfano wa 2
- Ugali ulinizuia kuinuka
- Baridi kali ilimkaribisha
(vi) Mubalagha
- Hii hutia chumvi kuhusu uwezo wa viumbe, tabia zao na kuhusu sifa zao kwa madhumuni ya kuchekesha au kusisitiza.
Mfano:
o Loo! Hebu mwangalie mrembo yule! Ana mlima wa kiuno.
o Tulimlilia Nyerere hadi kukawa na bahari ya machozi.
(vii) Metonimia au Taashira
Tamathali hii ni jina la sehemu ya kitu kimoja au la kitu kidogo kinachohusiana na kingine kikubwa hutumiwa kuwakilisha kitu kamili.
Mfano:
- Jembe huwakilisha mkulima
- Mvi – mzee
- Kalamu – mwanafunzi
- Ua – mwanamke mzuri
- Tabasamu – furaha
(viii) Taniuba
- Hii ni tamathali ambayo jina la mtu binafsi hutumika kwa watu wengine wenye tabia, mwenendo hali au kazi sawa na mtu huyo.
Mfano: -
o Yesu - Mkombozi
Yesu wa kwanza wa Afrika alikuwa Kwame Nkrumah.
o Amini- Uasi
o Maamini wengi wa Afrika ndio wanayorudisha nyuma mapinduzi ya waafrika.
(ix) Msisitizo bayana
- Hii husisitiza maana ya sentensi kwa kutumia kinyume
Mfano:
o Mwanadamu hupanga, Mungu hupangua
o Alikuwa msichana mzuri, ukimwangalia kwa mbali huwezi kujua anakuja au anakwenda.
(x) Ritifaa
- Ni tamathali ambayo mtu huzungumza na kitu au mtu ambaye husikiliza katika fikra tu
Mfano: -
- Amini umekwenda kufa, ametangulia
- Ewe mwanangu Hamisi, lala vyema humo tumboni mwa mama yako Ashura. Napenda ukazae siku zako zikifika ili mje kuishi katika mtaa huu wa Magila hapa kariakoo
(xi) Tahaini
- Usemi huu unasisitiza jambo kwa kutumia maneno ukinzani
Mfano: -
- Amekuwa mrefu si mrefu, mfupi si mfupi ni wa kati
- Usimwamini mtu yu acheka machoni rohoni ana roho mbaya
- Mweupe si mweupe, mweusi si mweusi ni maji ya kunde.
(xii) Takriri
- Ni kurudiarudia kwa neno, sentensi au kwenye usemi kwa nia ya kusisitiza au kupamba kazi ya fasihi
Mfano:
- Ndo! Ndo! Ndo! Si chururu
- Haba na haba hujaza kibaba
- Dunia ni ngumu jamani ni ngumu, ni ngumu, ni ngumu mpaka basi
(xiii) Mdokezo-
Msemaji au mwandishi huacha maneno bila kukitaja kitu au maneno ambayo kwa kawaida yanaeleweka na kuweza kujazwa kwa ubunifu.
Mfano: -
Ali alipokuwa analia alisema
(xiv) Tahtiti
- Ni mbinu ambayo mwasilishaji wa kazi ya fasihi anauliza swali wakati jibu analo, na hufanya hivyo kwa lengo la kusisitiza jambo kuleta mshangao n.k
Mfano: -
- Asha amefariki?
- “Amina na uzuri wake amekufa? Lo! Amina ametutoka? Hatakuwa nasi tena? Maskini!”
(xv) Nidaa
- Ni mbinu inayonesha mshangao au kushangazwa kwa jambo fulani na huambatana na alama ya kushangaa.
Mfano: -
- La hasha! La haula! Loo!
- Zaituni mpenzi wangu! Ningekuwa na uwezo ningekuandalia harusi ya ndovu kumla mwanawe.
(xvi) Onomatopia / Tanakali sauti
- Ni mbinu ya kuiga sauti za mlio wa vitu mbalimbali milio hii ni ya wanyama, magari, vitu n.k
Mfano: -
- Alitumbukia majini chubwi!
- Alidondoka chini puu!
7. Taswira
- Ni picha zinazojitokeza baada ya matumizi mbalimbali ya semi na ishara. Matumizi mazuri ya taswira na ishara hutegemea ufundi wa mwandishi wa kuweza kuchota mambo mbalimbali yanayomzunguka yeye na jamii yake na pia kutoka katika historia na sehemu zingine za maisha.
Kuna aina tatu za taswira
(i) Taswira za hisia
(ii) Taswira za mawazo / kufikirika
(iii) Taswira zionekanazo
I. Taswira za hisia
- Hizi zina nguvu kubwa ya kuganda akilini na kunasisha ujumbe wa mwandishi kwa wasikilizaji au wasomaji. Hizi hushughulikia hisia za ndani na kuweza kumfanya msomaji au msikilizaji awe na wasiwasi, aone woga, apandwe na hasira, asikie kinyaa n.k
Mfano: -
- Akidharau! Siwezi kula chakula kama hicho! Rojorojo kunyororoka kama limbwata, mfano wa kohozi lenye pumu, liingie katika koo langu lililozoea kuku kwa mrija”
- Kwa maelezo hayo yanaweza kumfanya mtu akinai na kutapika.
II. Taswira za mawazo/ kufikirisha
- Hizi zinatokana na mawazo, mawazo hayo yanayohusu mambo yasiyoweza kuthibitika.
- Mambo kama kifo, pendo, uchungu, fahamu, sahau na raha n.k
Mfano: -
- “kifo umefanya nini? Umeninyang’anya penzi langu bila huruma kumbuka nilimpenda nikapoteza fahamu, kifo ukazidi kunidunga sindano ya makiwa”.
III. Taswira zionekanazo
- Picha hizo hujengwa kwa kutumia vielelezo tunavyovijua yaani vile vinavyofahamika katika maisha ya kila siku
Mfano: -
- “Dakika haikupita, mijusi wawili waliokuwa wamebanana walipita haraka. Midomo yao ilikuwa myekundu. Ghafla walikutana na nyoka aliyeonekana mnene tumboni, hapana shaka alikuwa amekula mnyama”
UCHESHI
- Ni mbinu ya kifani ambayo wasanii hutumia katika kazi zao za fasihi kuzichekesha hadhira zao au walau kuzifanya hadhira hizo zitabasamu. Mbinu hii ya ucheshi hutumiwa na wasanii mbalimbali kwa makusudi mbalimbali.
- Wengine hutumia ucheshi ili kuwafurahisha wasomaji wa kazi zao.
- Ili kuondoa uchovu kwa hadhira zao
- Ili kukejeli katika kazi zao.
Upeo/ kelele katika maigizo
- Ni ile inayokidhi haja ya hadhira inayopokea kazi hiyo katika sehemu hizi watazamaji hupata majibu muhimu ambayo igizo/ onesha huwa imeyachelewesha kwa kutumia mbinu kadhaa kama vile tabaruki, mbinu rejeshi n.k
- Sehemu hizi mara nyingi husisimua watazamaji kwa hali ya juu sana . katika maigizo, watendaji hujenga migogoro ambayo hujitokeza na kukua jinsi kazi hizo zikuavyo zenyewe. Kipeo hutokea pale wanapotoa suluhisho la mgogoro katika onesho lake
Hata hivyo uamuzi huwa sehemu fulani ya onesho na kipeo hutegemea watazamaji wanaohusika.
Wakati mwingine hutokea kusiwe kabisa na kipeo katika onesho fulani.
Maudhui
- Ni jumla ya mawazo yote yanayozungumziwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo.
- Uhakiki wa maudhui katika maigizo huzingatia vipengele vifuatavyo: -
(a) Dhamira
- Hili ni wazo kuu au mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika onesho fulani.
- Hapa kuna dhamira kuu na dhamira ndogondogo. Hizi dhamira hukuzwa na matendo na mazungumzo ya wahusika kuanzia onesho la kwanza mpaka la mwisho.
(b) Falsafa
- Huu ni mwelekeo na imani ya msanii. Falsafa ni kazi ya sanaa inatakiwa ichambuliwe kwa kina kuzingatia jinsi kazi hiyo inavyoutazama ulimwengu unaoihusu na kueleza ukweli juu ya mambo mbalimbali. Ukweli huu lazima uhusishwe na binadamu. Falsafa ya msanii ndiyo inayotupatia mtazamo na msimamo wa msanii.
(c) Ujumbe na maadili
- Ujumbe katika maigizo ni yale mafunzo mbalimbali tunayoyapata baada ya kuona na kusikia igizo /onesho fulani.
Ujumbe huambatana na maadili mbalimbali.
(d) Migogoro
- Ni mivutano mbalimbali inayojitokeza katika maigizo. Migogoro hiyo inaweza kuwa kati ya mtu na mtu, familia na familia, tabaka na tabaka n.k migogoro hii mara nyingi hujitokeza katika mahusiano ya jamii ambapo yaweza kuwa migogoro ya kisiasa, uchumi, kiutamaduni au migogoro ya kinafsi.
- Kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa wakati wa kuchambua maudhui ya igizo fulani, maswali mbalimbali yanaibuka
o Je, msanii anatueleza nini?
o Msanii humtungia mtu wa tabaka gani?
o Anamtukuza nani?
o Anambeza nani?
o Msanii anatutaka tuchukue hatua gani katika utatuzi wa matatizo anayoyashughulikia katika kazi yake.
o Je, onesho hilo linachangia nini kwenye maudhui na dhamira?
UHAKIKI WA TANZU YA SEMI
SEMI
- Ni kauli za fasihi simulizi ambazo ni fupifupi zenye kutumia picha, tamathali za semi na ishara.
- Aghalabu ni mafunzo yanayokusudiwa kubeba maudhui yenye maana zinazofuatana na ishara mbalimbali za matumizi.
METHALI
- Ni semi fupifupi zenye kueleza kwa muhtasari, fikra au mafumbo mazito yanayotokana na uzoefu wa jamii.
- Mara nyingi mawazo hayo huelezewa kwa kutumia tamathali hasa sitiari na mafumbo. Methali ni kipera tegemezi kwasababu kutokea kwake kunategemea fani nyingine
Mfano: -
- Katika majadiliano mazito/katika muktadha maalumu wa jamii.
Vipengele vya fani
(a) Muundo
Methali mara nyingi huwa na mwenendo wenye sehemu mbili sehemu ya kwanza huonesha wazo fulani sehemu ya pili hukanusha wazo hilo.
Mfano: -
- Bandu bandu humaliza gogo
- Tamaa mbele mauti nyuma
- Haba na haba hujaza kibaba
Sehemu ya kwanza inakuwa ndefu kuliko sehemu ya pili na huwa ni kwasababu ni chanzo au kiini cha methali na kama ni chanzo cha methali inabidi ifafanue kwa kina kitu ambacho kinatendeka.
Sehemu ya pili ni fupi kwa sababu ndipo kwenye matokeo au jibu la matendo / maana ya sehemu ya kwanza.
Matumizi ya lugha
Methali hutumia tamathali za semi na kila methali ina sitiari kwa kiasi fulani na mara nyingi sitiari hutumika ili kuzipima sehemu mbili na kuzilinganisha kwa jambo ambalo lote huzingatia.
Sitiari
Hizi hulinganisha kitu na kingine kwa kuvifanya viwe sawa bila kutumia viunganishi
Mfano: -
- Ujana ni moshi, ukienda haurudi
- Mgeni ni kuku mweupe
- Kufa kikondoo ndio kufa kiungwana
- Mke ni nguo mgomba hupaliliwa
Tashihisi
Hizi ni tamathali ambazo vitu hupewa uwezo wa kutenda kama mtu
Mfano: -
- Kiburi si maungwana
- Siri ya mtungi ajuae kata
Kejeli
Methali nyingi huwa na kejeli katika maudhui yake.
Mfano: -
- Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti
- Ganda la mua la jana chungu kaona kivuno
Tashbiha
Tamathali hii hulinganisha vitu kwa kutumia viunganishi
Mfano: -
- Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza
- Mtoto wa nyoka ni nyoka
- Kawaida ni kama sheria
Msisitizo bayana
- Hii inaonesha ushindani wa mawazo. Hii inasisitiza maana ya sentensi kwa kutumia kinyume.
- Katika methali kuna aina mbalimbali za msisitizo
Mfano: -
- Msisitizo awali
Methali zenye tamathali ya aina hii hurudia neno moja mara mbili ili kusisitiza dhana fulani au onyo fulani .
Mfano: - Hayawi hayawi huwa
- Hauchi hauchi unakucha
- Mzaha mzaha hutumbua usaha
Msisitizo utatu
Methali za aina hii huwa na neno moja linalojirudia mara tatu kutoka methali moja
Mfano: -
- Mla mla leo, mla jana kala nini
- Awali ni awali, hakuna awali mbovu
Tamathali zinazokinzana
Hapo methali hubeba jozi za maneno yanayokinzana. Kuna tamathali zinazokinzana kwa kuingiliana na zile ambazo zina ikinzani wa pekee.
AINA ZA UKINZANI
(a) Ukinzani mwingiliano
- kukopa harusi kulipa matanga
- kizuri chajiuza kibaya chajitembeza
(b) Ukinzani pekee
- Mtu hakatai wito, hukataa aitiwalo
(usikatae wito,kataa maneno)
- Upendalo hupati, hupata ujaliwalo
- Simba mwenda pole,ndiye mlanyama.
Takriri
Hizi ni methali ambazo hujirudia rudia kwa ajili ya kusisitiza jambo
Mfano: -
- Asiyejua maana haambiwi maana
- Kokoto huzaa kokoto
- Mtoto wa nyoka ni nyoka
- Haba na haba hujaza kibaba
- Heri kujikwaa guu kuliko kujikwaa ulimi
Mbinu nyingine za kisanaa
(i) Onomatopea (tanakali sauti)
Ziko sauti zinazoiga sauti mbalimbali
Mfano: chururu si ndo! ndo! ndo!
(ii) Mfululizo sauti
Methali za aina hii zinabeba sauti maalumu mara nyingi hutawaliwa na herufi kama “ha” “ba” “pa”
Mfano: -
- Haba na haba hujaza kibaba
- Haraka haraka haina Baraka
- Padogo pako si pakubwa pa mwenzio
(iii) Maswali
- Baadhi ya methali hujenga sanaa yake kwa kuuliza maswali kimsingi maswali hayo hayahitaji majibu lakini jambo hili linakusudiwa kulengwa kwa hadhira na kufika huko.
Mfano: -
- Pilipili usizozila zakuwashia nini?
- Umekuwa bata akili kwa watoto?
- Angurumapo simba mcheza ni nani?
(iv) Mchezo wa maneno
Methali nyingine hucheza na maneno huleta maana mahsusi hasa kutoa maonyo
Mfano: -
- Ukiona neno usiseme neno, ukinena neno utapatwa na neno.
- Pema japo pema ukipema si pema tena.
(v) Picha au taswira katika methali
Sifa ya methali ni kule kujenga picha au taswira ambazo huchotwa katika mazingira. Picha hizo zaweza kuhusu wanyama, ndege, samaki, wadudu, mazimwi.
(a) Picha za wanyama
- Paka akiondoka panya hutawala
- Mzoea punda hapandi farasi
(b) Picha za wadudu
- Ukitupa jongoo tupa na mti wake
(c) Picha za ndege
- Kuku mwenye watoto halengwi jiwe
- Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake
(d) Picha za samani
- Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake
- Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti
- Chanda chema huvikwa pete
(e) Picha za silaha
- Vita vya panga haviamuliwi na fimbo
- Mshale kwenda msituni haukupotea
(f) Picha za matunda
- Mchagua nazi hupata koroma
- Koko haudai mai (maji)
(g) Picha za viungo vya mwili
- Ulimi unauma kuliko meno
- Heri kufa macho kuliko kufa moyo
- Kinywa jumba la meno
- Kifo cha mdomo mate hutawanyika
Wahusika
Wahusika katika methali ni muhimu kwa sababu hawa ndio wanaojenga kazi hii, wahusika wake ni binadamu na wako wa aina mbili.
Mtoa methali na wasikilizaji
Mazingira
Methali hufuatana na mazingira ya watu pamoja na silka.
Ni vigumu kwa mtu kupata uzito wa maana au jibu na dhamana za picha zilizotumika katika methali iwapo mtu huyo hana asili mahali methali ilipozaliwa
UHAKIKI WA VITENDAWILI
Kitendawili ni usemi uliofumbwa ambao hutolewa kwa hadhira ili ufumbuliwe. Fumbo hilo kwa kawaida huwa linafahamika katika jamii hiyo na mara nyingi lina mafunzo muhimu kwa washiriki mbali na kuwachemsha bongo zao.
Vitendawili ni sanaa inayotegemea uwezo wa mtu kutambua kuhusisha na kulinganisha vitu vya aina mbali mbali vilivyomo katika maumbile.
Ni sanaa inayotendwa inayojisimamia yenyewe hivyo ni tofauti na methali ambazo ni sanaa tegemezi au elezi.
VIPENGELE VYA FANI KATIKA VITENDAWILI,
Miundo
Vitendawili vina miundo yake maalumu tofauti na tanzu nyingine za fasihi simulizi.
Muundo wa kitendawili unaweza kuwa kama ifuatavyo
Kitangulizi (mtambaji au mtendaji)
Mfano: -
- Kitendawili......... tega ........(mtegaji)
- Kitendawili swali / fumbo lenyewe
- Swali la msaada (nini hicho)
- Kichocheo...toa mke, toa mji, lipa mbuzi au lipa binti
- Jibu lenyewe
Hii inaonesha kuwa vitendawili ni fumbo au swali linalohitaji jibu
- Mume mrefu lakini mke mfupi, lakini wanashirikiana sana
- Mtegaji hujibu “mchi na kinu”
Mtindo
Kitendawili kina mtindo wa majibizano (dayolojia) kati ya mtendaji (mtambaji) na mtegaji (wasikilizaji)
Mtambaji hutoa kitangulizi kwa kusema “kitendawili” hujibu “tega”, kisha hutoa kitendawili chenyewe yaani swali au fumbo lenyewe.
Wasikilizaji wanatakiwa kutoa jibu na wakishindwa wanamshawishi mtambaji atoe jibu mwenyewe kwa kumpa mji yaani kichocheo.
Namna na aina ya kichocheo hutegemea sana mahali na mahali.
Matumizi ya Lugha.
Vitendawili hutumia lugha ya sitiari na mara nyingi lugha hii huwa na aina ya ashoiri ndani yake. Vilevile vitendawili vya Kiswahili vina utajiri mkubwa ndani yake na lugha.
TAMATHALI ZA SEMI
Sitiari
Mbinu za kulinganisha vitu pasipo kutumia viunganishi
Mfano: -
- Samaki wangu anaelea kimgongo mgongo (marehemu)
- Nyumba yangu haina mlango (yai)
- Mwarabu wangu mkali sana ukimshika hashikiki hana panga, hana shoka, hana kisu, hana mshale (moto)
- Nyumba yangu ina mlango mdogo
Tabaini
Kusisitiza jambo kwa kutumia maneno kinzani
Mfano: -
- Yule anatuona sisi hatumuoni (Mungu)
- Futi kufunika futi kufunua (nazi fuu, nazi maji)
- Mkubwa ananiamkia, mdogo haniamkia (kunde kavu na mbichi)
Kejeli na dhihaka
- Uzi mwembamba umefunga dume kubwa (usingizi)
- Upara wa mwarabu unafuka moshi (chai, maziwa, ugali)
- Kitu kidogo kimemtua mfalme kibini (hajandogo)
- Mama mtu mweusi, watoto wekundu (pilipili)
Tashihisi
Mfano: -
- Popo mbili zavuka mto (macho)
- Popote niendapo ananifuata (kivuli)
- Ninapompiga mwanangu watu hucheza (ngoma)
Takriri
Mfano: -
- Huku fungu huku fungu katika bahari (nazi)
- Mama kazaa mtoto na mtoto kazaa mtoto (kuku na yai)
- Futi kufutika futi, futi kafutika futi (nazi – kumbi) (nazi na tui) (maji ya nazi)
- Juu go, chini go katikati gogo (kinywa mdomo na ulimi)
Mbinu nyingine za kisanaa
Onamatopea (tanakali sauti)
Mfano: -
- Huku pi na kule pi (mkia wa kondoo atembeapo)
- Chubwi aingia chubwi katoka (jiwe majini)
- Pa funua pa funika (nyayo wakati wa kutembea)
- Enda “parara” (kuti la mnazi)
- Pakacha tiii! ( ugonjwa wa matende)
Taswira au picha
Katika vitendawili kuna matumizi ya picha za miti, viungo vya mwili, wanyama, vitu.
Mfano: -
- Kuku wangu kataga mibani (nanasi)
- Mzazi ana miguu bali mzaliwa hana (kuku na yai)
- Mti mmoja una matawi saba, manne mabichi, pembe mbili, matatu makavu na mkia mmoja (Jani lenye wazimu)
- Wanangu wanne lakini hawakamatani
Kinaya
Hutumiwa kueleza usemi ambao una maana ya kinyume na usemavyo kijuujuu
Mfano: uzi mwembamba umefunga dume kubwa.
Ucheshi/ vichekesho
Kuna vitendawili ambavyo huweza kusababisha ucheshi kwa msomaji ucheshi huu hutokana na uhusiano uliopo kati ya kitendawili fulani na maana yake au kile kinachoongelewa nacho.
Mfano:-
- Mwarabu kavaa kilemba
- Nimemwona bi kizee amejitwika machicha (mvi)
- Baba apiga mbizi, akiibuka ndevu zimegeuka nyeupe (mwiko)
Utata
Ni ule ugumu uliopo wa kuamua maana inayokusudiwa au jibu la kitendawili, kuna baadhi ya vitendawili ambavyo vina majibu mengi, jibu sahihi au linalokusudiwa hutegemea mazingira, mandhari, utamaduni,wakati n.k.
Mfano: -
- Inachurura inaganda (Asali/ gundi)
- Gari la kila mtu (kifo, jeneza, miguu)
- Hamwogopi mfalme wala bawabu (njaa/ shida/ kifo)
UHIFADHI WA KAZI ZA KIFASIHI SIMULIZI
Kazi za fasihi simulizi huweza kukusanywa kwa kusikiliza wasanii wakizisimulia, kuzitamba kazi hizo mfano mkusanyaji anaweza kujiunga na wachezaji hao ambao huwa wanapiga soga na kusimulia hadithi mbalimbali. Hivyo msikilizaji anaweza kuziandika au kuzihifadhi kwa njia bora na ya kudumu zaidi.
Kuwatembelea wazee ambao ni mashuhuri katika kutamba hadithi, kughani mashairi au kutumia misemo na methali ili kuwasikiliza na baadae kuzikusanya kazi hizo tayari kwa kuzihifadhi.
Kuwasikiliza wasanii wakisimulia na kuzitamba kazi zao hivyo fanani anaweza akasikiliza, akaziandika au akazirekodi tayari kwa kuzihifadhi kwenye kichwa, kinasa sauti, filamu au maandishi.
Kuna njia mbalimbali zinazotumika katika kuhifadhi kazi za fasihi simulizi.
Kichwa
Maandishi
Kanda za sauti (tepurekoda) kanda za kunasia sauti
Kanda za video, televisheni na filamu za sinema.
KICHWA
Tangu zamani uhifadhi wa fasihi simulizi upo katika kichwa cha fanani na kutolewa kwa masimulizi. Jambo hili limekuwa likifanyika kwa muda mrefu sasa, kutokana na kuhifadhiwa kichwani ndio maana fasihi simulizi ilikuwa ikirithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.
Ubora wake
Bado fasihi simulizi inapohifadhiwa kichwani huendelea kuwa hai kwani hadhira na fanani huwasiliana ana kwa ana.
Hadhira huweza kumpongeza au kumhoji fanani papo kwa papo.
Udhaifu
Fasihi simulizi kuhifadhiwa kichwani husababisha matatizo ya kupoteza kumbukumbu kutokana na kumbukumbu za akilini kufifia au kupotea hali hii ikitokea simulizi hiyo hupotea kabisa.
Kubadilisha mambo muhimu katika simulizi
Fasihi simulizi hupoteza kiini chake au ukweli wake pindi tu msimuliaji apotezapo kumbukumbu ya anayosimulia
(fanani akifa / akirukwa na akili)
UHIFADHI KATIKA MAANDISHI
Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia fasihi simulizi inahifadhiwa katika maandishi kwa ajili ya kumbukumbu za baadaye.
Ubora wake
Kazi ya fasihi simulizi ikihifadhiwa katika njia hii haipotei au haibadiliki. Ni njia yakutunza kumbukumbu ya kudumu
Udhaifu wake
- Katika maandishi fasihi simulizi haina sauti hivyo msomaji atie sauti au madaha yote mwenyewe. Hali hii inaweza kusababisha au kufikisha ubora wa kazi hiyo.
- Pia katika maandishi wahusika hawaonekani kwahiyo hadhira hushiriki kwa kuona maandishi
- Vilevile fasihi simulizi hupungua uhasilia kwani si hai tena uhai wa fasihi simulizi hujikita katika utendo na ushiriki wa fanani na hadhira.
- Huwa mali ya wachache
Fasihi simulizi tangu mwanzo ilikuwa inamilikiwa na jamii nzima kwa kuweka katika maandashi inakuwa ni mali yamsanii na hadhira yake inakuwa finyu. Hii ni kutokana na kwamba lazima ujue kusoma na kuandika ili uweze kujua kazi ya fasihi ilivyoandikwa.
- Haibadiliki kulingana na wakati na mazingira. Toka mwanzo fasihi simulizi ilikuwa ikibadilika kutokana na mazingira kwa hiyo ikibadilika mazingira nayo hubadilika na mambo yaliyosimuliwa.
- Ina gharama kwani waandishi hununua kalamu na karatasi pamoja na zana mbalimbali ili kuweza kutoa kitabu.
UHIFADHI WA VINASA SAUTI
Hizi ni zana zitumikazo kurekodi sauti mfano; tepurekodi,kanda za muziki na sauti CD n.k
Ubora wake
- Katika njia hii ukweli wa sanaa ya kazi haitabadilika. Sauti ya wahusika halisia itaendelea kusikika kama ilivyotolewa hivyo fasihi simulizi haipotei wala kubadilika badilika.
- Njia hii inatunza kumbukumbu.
Udhaifu wake
- Utendaji wa wahusika hawaonekani kwahiyo hadhira itashiriki kwa kusikiliza kanda kwahiyo sio hai.
- Haitabadilika kulingana na mazingira na wakati. Kubadilika kwa mazingira hubadilisha mambo yanayosimuliwa lakini fasihi simulizi iliyorekodiwa kwenye vinasa sauti ikisharekodiwa haibadiliki. Hivyo kutaendelea na mabadiliko ya nyakati na hali halisi ya wakati huo
- Ni ghali mno. Fasihi simulizi iliyorekodiwa katika kanda ni ghali mno kiasi kwamba huwa shida kwa hadhira kuipata na pia kuirekodi huitaji pesa, hivyo ni ngumu kuhifadhi fasihi simulizi kwa njia hii.
KANDA ZA VIDEO, RUNINGA, TANAKILISHI NA FILAMU ZA SINEMA
Kanda za video hurekodi sauti na sura. Picha hizo huoneshwa kwenye video na runinga. Picha za sinema hupigwa kwa aina maalumu za kamera ambazo huoneshwa na projecta na huonekana watu na matendo yote yatendwayo. Hivyo kwa kutumia filamu za video tunaweza kuhifadhi na kuonesha kazi za fasihi simulizi.
Ubora wake.:
- Huweza kutunza kumbukumbu za muda mrefu na zilizohifadhiwa kwa njia hii hazipotei au kusahaulika.
Udhaifu wake
- Haibadiliki kutokana na mazingira na nyakati kwa kubadilika kwa mazingira hubadili usimulizi lakini njia hii haiwezi badili usimulizi pindi tu ukisharekodiwa hivyo kutoonesha uhalisia wa mazingira na nyakati.
- Ni ghali mno. Fasihi simulizi iliyorekodiwa katika filamu au redio huwa aghali mno wakati wa kurekodi. Pesa nyingi huitajika ili uweze kurekodiwa na vifaa vitumikavyo ni aghali sana na hata ikisharekodiwa bado huuzwa aghali ili uweze kurudisha gharama zilizotumika katika kurekodi, hivyo huwafikia wale tu wenye uwezo wa kifedha. Hivyo si mali ya jamii nzima.
UMUHIMU WA KUHIFADHI KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
- Kwa kuwa fasihi simulizi imejikita kwenye shughuli na tabia za kila siku za jamii ni wazi kuwa fasihi simulizi ni hai. Kwa hiyo ni vyema tukahifadhi fasihi simulizi za kale na sanaa.
- Lengo kuu la kuhifadhi fasihi simulizi na kale ni sisi kuzifanya zisipotee.
- Pia ili tuweze kutumia mali za jamii yetu kwa kuwa kuhifadhi nyimbo ni kazi nyingine za kisanaa ni tuzo na kumbukumbu tosha kwa vizazi vijavyo.
- Sanaa ni mali ya jamii ya kizazi kijacho kitatumia mali hizi zilizotumiwa kujifunza, kuburudika, na hata kugundua sanaa zaidi kwani tayari wana msingi fulani wa kuanzia.
UTUNGAJI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
Kwa kawaida mshairi anapotunga shairi / wimbo hutoa hisia yake au maoni yake juu ya jambo fulani. Mambo hayo hutolewa kufuatana na jinsi anavyoliona jambo lile na anavyoamini kuhusu jambo lile. Hii ina maana kwamba maoni yale hutolewa kulenga na imani ya mshairi mwenyewe. Imani ya mshairi ndiyo inayojenga msimamo wake katika maisha, yaani falsafa yake.
Mtunzi yeyote katika ushairi, utunzi wake huwa umezingatia vipengele viwili muhimu navyo ni fani na maudhui.
Kwa ujumla mtunzi yeyote wa tanzu ya fasihi simulizi huzingatia vipengele hivi viwili katika utunzi wake.
KANUNI ZA UTUNZI WA USHAIRI WA FASIHI SIMULIZI
Maudhui
- Katika kipengele cha maudhui mtungaji wa mashairi anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo katika kufanikisha lengo la utunzi wake.
Lengo la mshairi
- Kabla hajaanza kutunga shairi lazima ujue sababu za kutaka kueleza hayo unayo taka kueleza kwa maana ya kwamba lazima uwe na jambo lililokusukuma kutunga wimbo au shairi.
- Mshairi anapotunga huwa na kitu maalum akisemacho
- Huwa na ujumbe anakusudia kuwasilisha kwa jamii yake
- Kuelewa vizuri jamii aliyoiandikia
- Mtunzi wa ushairi asitunge bila kuwa anamkusudia mtu au watu fulani. Watu hao waweza kuwa marafiki, watawala, jamaa, maadui au yeye mwenyewe n.k.
- Utakapo mfahamu unaye muandikia itakusaidia kujua utunzi wake kwa sababu utajua imani na taratibu mbalimbali za maisha ya huyo mtu na hii itakufanya utunge vizuri kazi yako na humuathiri vilivyo mlengwa wako.
Kujua mipaka ya uhuru wa uandishi wako
- Mwandishi yeyote huweka mipaka katika uandishi wake .Kwa hiyo mtunzi yoyote Yule atake au asipende hujikuta amewekewa mipaka katika utunzi wake. Hivyo Kama mtunzi yakupasa utambue mipaka yako kwani pasipo kufanya hivyo utasababisha matatizo. Iwapo utavuka mipaka vizuri kutasaidia kuyaandika yale unayoyataka kwa ustadi na kufikisha ujumbe utakao kusudiwa bila matatizo.
Kuoanisha dhamira na wakati
- Ni muhimu mtunzi kuandika jambo hilo ambalo anafikiri jamii yake inahitaji kwa wakati huo. Mfano mtunzi anaweza kuandika juu ya uongozi mbaya, UKIMWI, madawa ya kulevya kwani mambo hayo ndiyo yanayo tugusa katika jamii zetu.
- Kwa hiyo kama mtunzi ataandika mambo ambayo yanaenda na mahitaji ya jamii kwa kipindi hicho basi atapata hadhira kubwa kuliko akiandika mambo yaliyopitwa na wakati. Kwa hiyo basi mtunzi lazima awe na jambo kuu moja ambalo analitafutia ujumbe mbalimbali na mawazo madogo madogo ambayo yatakayo kamilisha ujumbe huo .
Fani
Mambo muhimu ya kuzingatia
Kuoana – Utungo wa ushairi ni masimulizi ya tukio fulani au maelekezo juu ya jambo fulani. Hivyo basi ni kwamba masimulizi au maelezo hayo yanahitaji mtiririko wenye mawazo mazuri yenye kuoana
Utungaji ambao hauna mpangilo mzuri huwa na matatizo mbalimbali kama vile kukosa kuelewa kile asemacho.
Upangaji mbaya wa mawazo husababisha shairi kukosa ladha na hivyo msikilizaji hukosa hamu ya kusikiliza
Kutotumia mitindo inayofaa
- Uchanganuzi wa aina ya shairi atakao tumia mtungaji unategemea sana dhamira iliyo kusudiwa pamoja na lengo alilonalo msanii mwenyewe.
Mfano:-
- Unapo taka kuzungumza mambo ya kihistoria kwa urefu na upana inabidi atumie utam wa utenzi kuliko wimbo au ushairi kwani tenzi inaweza kutungwa beti nyingi kulingana na kitu kinacho zungumziwa
Utenzi wa lugha
- Lugha ni kipengele muhimu sana katika ushairi. Mtunzi wa ushairi katika kipengele cha lugha ni lazima awe makini kwani lugha isipo kuwa tamu husababisha hata maudhui kuwa chapwa. Mtunzi lazima azingatie mambo yafuatayo katika kipengele cha lugha.
Lugha ya kishairi
- Ushairi una lugha yake tofauti na lugha itumiwayo katika mazingira mengine ya kawaida kwani lugha ya ushairi ni ya kutumia maneno machache ya mkato na siyo mengine.
Matumizi ya picha
- Hii husaidia kuvuta taswira ya mambo yanapo ongelewa na kukamata akili ya msikilizaji kwa namna ya ajabu. Pia husaidia sana kuvuta hisia na kuleta mguso wa hali ya ajabu na hisia za juu kwa msikilizaji.
Matumizi ya tamathali za semi
- Hizi hupanua au hubadilisha maana ya halisi au ya kawaida za maneno ili kuleta maana maalumu iliyo kusudiwa na mtunzi . Mtunzi wa shairi atakapozijenga tamathali zake vizuri huipa uhai na uhalisia zaidi dhana inayo elezwa huiburudisha na kuzindua akili ya msikilizaji wa shairi na huacha athari ya kudumu katika hisia ya mawazo yake.
- Tamathali zinazotumika zaidi katika ushairi ni tashbiha, tashhisi, mbalagha, kejeli, sitiari n.k. Hivyo mtunzi wa shairi lazima atumie tamathali kujenga kazi yake.
Matumizi ya mbinu nyingine za kisanaa
- Kuna mbinu nyingine za kisanaa zinazo karibiana na tamathali za semi ambazo hutumika nsana katika utunzi wa mashairi. Mbinu ambnazo hutumiwa sana na ushairi ni takriri, tanakali sauti , ridhimu ( mapigo asilia ya lugha ) n.k. Kwa hiyo wakati wa kutunga msanii lazima azingatie mbinu kama hizi.
Matumizi ya nahau na misemo
- Hivi ni viungo muhimu katika lugha ya ushairi na kufanya lugha ya msanii au mwandishi fulani kuwa na mivuto mikubwa ya kisanaa, hivyo ni muhimu kuzingatia matumizi ya nahau na misemo.
Matumizi ya methali
- Methali hutumiwa sana na wasanii kwani hutumiwa sana katika kupitisha hekima na busara kwa jamii na pia hutumika kujenga na kupamba lugha.
Lugha ya wahusika
- Tunapozungumzia kuwa kuna lugha ya wahusika ina maana kuwa kama msanii amekusudia kutoa maonyo basi inambidi atumie lugha ya maonyo . Vilevile kama atatumia hadhira maalum basi lugha lazima ieleweke na hadhira hiyo.
Kuzingatia kanuni za uandishi
- Kuna kanuni ambazo zinatakiwa kufuatwa hasa unapotaka kutunga mashairi ya kimapokeo ambazo ndizo nguzo hasa za ushairi na pia kuna mambo mengine yanayo takiwa kufuatwa katika kutunga mashairi.
Kanuni za utunzi wa mashairi ya kimapokeo
1) Vina
- Katika ushairi vina ni ile mizani ya kati na ya mwisho yenye kufanana katika kila mstari wa ubeti. Katika tabia aghalabu vina hufuatana katika kila mishororo mitatu ya mwisho inaweza kubadilika.
2) Kituo
- Huu ni mstari wa mwisho katika kila ubeti wa ushairi. Kituo cha mstari kinaweza kuwa kimalizio au kiini kituo kinapo kuwa kimalizio kinatumika kulifunga na kukamilisha wazo moja katika kila ubeti. Na kinapokuwa kiini kina jitosheleza katika kila mwisho wa ubeti na kutaja kwa muhtasari jambo muhimu linalozungumziwa.
3) Kipande
- Hiki ni kisehemu kimojawapo katika visehemu viwili au zaidi katika kila mstari kutegemea na mtunzi mwenyewe alivyo amua kutunga kazi yake.
4) Mizani
- Ni jumla / idadi ya silabi zilizomo katika kila mstari wa ubeti mizani husaidia kuleta mapigo katika shairi na kufanya liweze kuimbika.
- Mara nyingi shairi la kimapokeo huwa na mizani 16 na lazima ifanane katika kila kila ubeti wa shairi lakini ushairi wa fasihi simulizi si lazima mizani ifanane sana.
5) Ubeti
- Hiki ni kifungu chenye kuleta maana kamili katika jumla ya vifungu ulivyo navyo kwenye shairi na ubeti hubeba wazo kamili katika shairi.
6) Urari
- Pia mtunzi lazima azingatie kuwa na urari na mawazo kati ya mstari na mstari au ubeti na ubeti kwani kuna baadhi ya watunzi hukosea au katika kazi zao kunakuwa hakuna urari wa mawazo au mawazo hayaoni.
7) Utoshelezi
- Mtunzi yeyote wa shairi la Kiswahili ni lazima azingatie utoshelezi wa ubeti kwani ni lazima kila ubeti ujitosheleze kimaana( ujumbe kabla hujaingia kwenye ubeti wa pili msomaji anapaswa awe ameelewa kitu gani kilichokuwa kinaongelewa kwenye ubeti wa kwanza na pia mshororo nao inabidi uwe ni wenye kiujumbe.
8) Kuwa na maana
- Pia shairi ni lazima liwe na maana kwani hili pia ni jambo la msingi katika ushairi kwani mtunzi anaweza kufuata kanuni zingine zote lakini bado shairi lake linaweza lisieleweke kwani alikuwa anataka hadhira yake ijifunze nini.
- Vilevile mtunzi anaweza akagundua beti Kama kumi lakini shairi linakuwa halina maana na msanii mwingine akafunga hata beti moja tu na shairi lake linakuwa na maana kamili na kuwa na ujumbe unaoleweka.
9) Muwala
- Ni ufuatanisho wa habari toka ubeti hadi ubeti. Mfano shairi lenye beti nane linaweza kuleta zama ukaona ubeti wa nne ungekuwa wa pili na wa pili labda ungekuwa mahali fulani au usinge kuwepo kabisa kutokana na mtiririko ulivyo kuwa. Haya yote ni katika kufanya miwala iwe mizuri katika shairi na hiyo ni moja ya kazi ngumu katika kutunga shairi la Kiswahili
10)Msisitizo
- Hii ni hali ya kushadadia kwa kiini cha jambo au dhamira kuu katika utungo huo kama tulivyo kwisha ona msisitizo katika shairi laweza kuwa wima au ulalo
- Baada ya kuona hizo kanuni za mtunzi na shairi tuangalie mambo mengine ambayo pia ni muhimu katika utunzi wa shairi ili liweze kuwa bora au zuri zaidi mambo hayo kama;-
I. Kutorudia maneno
- Shairi litapungua utamu kwa kurudia maneno. Msanii anaporudia neno moja katika kila ubeti husababisha shairi kukosa ladha na utamu, pia mtunzi huonekana kama hana ujuzi wa lugha.
Lakini kuna mashairi ya msisitizo ambayo toka ubeti wa kwanza mpaka wa mwisho huanza na neno hilo basi kama neno huanza na shida basi katika kila ubeti huanza na neno hilo hilo hiyo siyo kurudia maneno bali ni mtindo wa msanii.
II. Kichwa cha shairi
Kichwa cha shairi ni muhimu sana katika kufikisha ujumbe kwa msikilazaji kwa hiyo kama shairi halina kichwa basi linakuwa sio tamu. Shairi ambalo ni bora ni lile linalo kuwa na kichwa
Kutochanganya dhamira
Pia unapo changanya dhamira mbili au zaidi katika shairi moja hilo linakuwa shairi baya kwani unapo andika shairi inabidi uende na dhamira moja kuanzia ubeti wa kwanza mpaka wa mwisho ndipo shairi linapendeza sana na hii husaidia kueleweka kwa dhamira ya shairi.
Kunga
Siri ya shairi ni kulihifadhi lisiwe mbali sana. Ni kwamba mtunzi anapotunga inabidi asitumie lugha ya kashfa au ya matusi. Anaweza kutumia lugha ya mafumbo ili aweze kuyafumbua.
Matumizi ya tamathali za semi
- Hizi hupanua au kubadilisha maana za dhahiri au za kawaida za maneno ili kuleta maana maalum iliyo kusudiwa na mtunzi . Mtunzi wa shairi atakapo zijenga tamathali zake huipa uhai na uhalisia zaidi dhana inayoelezwa, pia huburudisha na kuzindua akili ya msikilizaji wa shairi na kuacha athari ya kudumu katika hisia na mawazo yake.
- Tamathali zinazo tumika katika ushairi ni tashbiha, tashihisi, kejeli, sitiari, n.k. Hivyo mtunzi wa shairi lazima atumie tamathali katika kujenga kazi yake.
Matumizi ya mbinu nyingine za kisanaa
- Kuna mbinu nyingine za kisanaa zinazo karibiana na tamathali za semi ambazo hutimika sana katika utunzi wa shairi . Mbinu ambazo hutumiwa sana na ushairi ni takriri, tanakali sauti(onomatopea), rithimu, mapigo asilia ya lugha n.k. kwa hiyo wakati wakutunga msanii lazima azingatie mbinu kama hizi.
Matumizi ya nahau na misemo
- Hivi ni viungo muhimu katika lugha ya ushairi na huifanya lugha ya msanii au mwandishi fulani kuwa na mvuto mkubwa wa kisanaa. Hivyo ni muhimu kuzingatia matumizi ya nahau na misemo.
Matumizi ya methali
- Methali hutumiwa sana na wasanii katika kupitisha hekima na busara kwa jamii na pia hutumika kujenga kejeli kwa kupamba lugha
UTUNGAJI WA MAIGIZO
- Mtungaji yeyote anapotaka kutunga maigizo kuna vipengele mbalimbali ambavyo jamii inapitia vizuri kazi yake na akaweza kubuni mbinu ambazo zitaifanya kazi yake ipendeze na kuvutia kwa hiyo itakidhi mahitaji ya jamii husika kwa kipindi hicho
Vipenngele muhimu vyaa kuzingatia katika utunzi wa maigizo
(a) Lengo la mtunzi
- Mtunzi lazima aandike maudhui yenye umuhimu katika jamii na yanayoendana na wakati. Msanii mzuri inabidi apange maudhui yake hata kama yakiwa yanahusu Tanzania ya zamani lazima yawe na umuhimu katika Tanzania ya leo . Pia anaweza akazungumzia masuala tofauti tofauti ambayo yanaleta maendeleo kwa jamii
(b) Hadhira inayoandikiwa.
Mtunzi lazima ajiulize anaandika kwa hadhira gani kwani hadhira atakayo iandikia ndiyo itakayo amua usanii ni nini na vipi jambo hili ni muhimu kwa mtunzi kwa sababu kufaulu au kutofaulu kwa igizo hutegemeana na hadhira yako itakavyo pokea hilo igizo litakalo oneshwa jukwaani. Msanii pia inabidi afahamu mawazo ya hadhira yake. Juu ya jambo analotaka kuwasilisha kama ni tofauti na mtazamo wake basi atumie mbinu itakayo shawishi wakubaliane nayo.
(c) Utenzi wa vitendo.
- Msanii anapotunga igizo lazima achague matendo ambayo yatasaidia kulijenga wazo lako. Wazo moja linalotokeza huwakilishwa na matendo mengi ambayo yatasaidia kufikisha ujumbe vizuri vile ulivyokusudiwa hadhira yake ipate kujifunza. Dhamira yake kuu ndiyo itakayo muwezesha achague matendo ya aina fulani.
(d) Ujengaji wa wahusika
- Wahusika wa maigizo inabidi wajengwe kutokana na msukumo na migongano iliyomo katika igizo. Maneno, mawazo na matendo yao yapate chanzo kutokana na migogoro hiyo. Kwa namna hiyo wahusika watapata uhalisia na kuvaa uhusika wa kuaminika katika jamii waliyotoka.
(e) Uteuzi wa maneno
- Mtunzi wa igizo anapaswa kuchagua maneno kwa uangalifu kwa sababu wakati mwingine mtunzi huwapa wahusika wake maneno mengi kiasi kuwa igizo linakuwa na maneno matupu kuliko vitendo kwani matendo yakiwa yamejengwa vizuri huleta maana husika kwa hadhira na maneno machache hupelekea igizo kuwa zuri na la kuvutia
(f) Uteuzi wa misukumo
- Msanii anapaswa achague misukumo itakayoweza kusababisha mitazamo isitokee. Na ili jambo litokee inabidi ajenge pande zote ziwe na misukumo yenye nguvu ambayo italeta matokeo na kama upande mmoja ni dhaifu basi hakuna jambo litakaloweza kutokoea.
(g) Matendo jukwaani
- Mtunzi anatakiwa achukue matendo ambayo yanaweza kuoneshwa katika jukwaa. Igizo lolote haliwezi kukamilika bila kuoneshwa jukwaani ili liweze kuonekana kwa hadhira.
- Mtunzi inabidi achague matendo ambayo yanaweza kuonesheka huku yakiambatana na mbinu zingine.
UIGIZAJI WA MAIGIZO JUKWAANI.
Maigizo yanapo kuwa yanaoneshwa kwenye jukwaa huonesha matendo ya binadamu na maisha wanayoishi kila siku iitwayo leo
Katika uigizaji wa maigizo mambo muhimu ya kuzingatia ni :
a) Jukwaa
- Katika maigizo lazima kuwe na jukwaa la kuigizia ambalo ni kitu muhimu katika tanzu hii. Zamani maigizo yalikuwa yanaigizwa nje lakini siku hizi hutumia majukwaa ya ndani.
- Hii ni kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia hata hilo jukwaa la ndani bado ni dhiki kuigiza katika jukwaa hilo
b) Mazungumzo
- Vile vile mazungumzo ya wahusika ni muhimu sana tofauti na maelezo ya mtunzi kwani husababisha igizo kuwa zuri na kuvutia machoni mwa watazamaji.
c) Mavazi
- Mavazi ya wahusika ni muhimu sana katika maigizo. Hii ni kwa sababu wahusika wanapo igiza wanatakiwa kuonesha watu walivyo wanavyoishi katika kipindi fulani cha historia au watakavyo ishi siku zitakazokuja.
- Hayo mavazi wanayovaa yaendane na uhalisia wa maisha ya jamii hiyo na kile kilichoigizwa.
- Pia maleba huonesha bayana tofauti za kitabaka zilizopo katika jamii. Kazi ya upambaji hufanywa na mpambaji wa jukwaa au mkurugenzi wa maigizo.
d) Vifaa vya kuigizia
- Vifaa vinavyotolewa na mtunzi kwa ajili ya kutumika jukwaani mara nyingi huwa na umuhimu. Mtunzi anatakiwa ahakikishe kwamba vifaa anavyo tumia mhusika aoineshe halisi ya lile jambo analowasilisha.
Mfano:-
- Igizo linataka kuonyesha watu wanavyoishi vijijini .
- Hivyo basi ni muhimu vifaa vinavyo teuliwa viwe na uhusiano barabara na uhalisia wa jamii iliyo teuliwa.
e) Jinsi ya kuigiza
- Wahusika wanatakiwa watende vitendo kwa hisia kuliko maneno. Mhusika anatakiwa afanye hivyo kama kweli yamemtokea yeye (kumgusa yeye mwenyewe) katika maisha yake kwa kufanya hivyo atakuwa amefanikiwa kuvaa uhusika na watazamaji wanapata hisia na kuzama katika kulitafakari hilo igizo.
Mfano :-
- Mtu anatakiwa aigize kama ana huzuni lakini yeye anatabasamu
f) Mpangilio wa maigizo
- Katika maigizo huwa na maonesho mbalimbali ambayo huweza kujisimamia yenyewe lakini wakati mwingine huingiliana na maonesho mengine kwa ajili ya kukamilishana. Mawazo hayo huweza kupangwa katika sehemu mbili mpaka saba na katika sehemu moja katika maudhui kadhaa hupatikana na h ndio hutupatia vitendo vya wahusika.
- Kwa hiyo kitendo kimoja hutupelekea jambo fulani na mambo yanapokuwa mengi sharti kuwa na uwiano katika kujenga migogoro mpaka kufikia kilele na kupata suluhisho la hiyo migogoro.
g) Maigizo katika maigizo
- Tanzu hii ya maigizo wakati mwingine inawezekana kukawa na igizo ndani ya igizo. Katika maigizo ya namna hii kuna igizo ndani ya igizo moja ambalo linakuwa ndani ya akili ya wahusika na mtunzi hupandisha jukwaani na kuoneshwa au watazamaji huingiziwa katika upande wa upili ambalo huwa na mambo yanayo shughulikiwa.
Mfano :-
- Mtu aliye kuwa maskini anakuwa tajiri mwanafunzi anakuwa daktari au profesa na kuonesha matendo ya huyo profesa na wakati ikiendelea hivyo moja huwa limegandishwa.
h) Mwisho wa mchezo.
- Mwisho wa uigizaji suluhisho linaweza kupatikana au lisipatikane kipindi cha nyuma mchezo ulikuwa hauishi hii ni kwasababu walikosa njia mbadala ya kuondokea jukwaani lakini siku hizi watunzi mbalimbali wanaweza kutoa masuluhisho na wakati mchezo unaishia waigizaji huondoka jukwaani kwa amani
KUIGIZA NGONJERA.
- Ngonjera ni aina ya ushairi zinazowasilishwa kwa kutumia mazungumzo ya majibizano baina ya watu wawili au zaidi.
- Jambo kubwa kabisa katika ngonjera ni kwamba zenyewe husemwa haziimbwi kifani na kimaudhui hufuata taratibu zote za ushairi
Vipengele muhimu vya ngonjera
(i) Dhamira maalumu.
- Ngonjera huwa na dhamira maalum yaani hujibu swali. Ngonjera hii imeandikwa juu ya nini? Je ina usemi kwa waangaliaji wake?
(ii) Wahusika
- Pia ngonjera huwa na wahusika inaweza ikawa na wahusika wawili au zaidi mpaka wahusika wanne. Mfano inaweza kuwa na wahusikia wawili, mmoja mjuaji na mwingine ni maalum asiyejua kitu chochote na mwisho wa ngojera yule maalumu anakuwa amekubaliana na yule mjuaji.
- Watunzi wengi siku hizi wameongeza wahusika zaidi ya wawili kwa sababu mchezo hauwezi kuchezwa bila wahusika kwa maana wao ndio wana himili hisia zao wanaakili na kutimiza hizo akili zao katika kutatua migogoro inayo wakabili.
- Waandishi hugawanya wahusika wao katika sehemu mbili mhusika mkuu na wahusika wadogo. Mara nyingi mhusika mkuu huwa mwema na wahusika wadogo wadogo huwa wabaya lakini mtindo huo sio mzuri ni dhaifu.
(iii) Migogoro
- Moyo wa mchezo wowote wa kuigiza uwe ni ngonjera au maigizo upo katika migogoro inayojengwa na mjuaji anajibu kumdokeza yule asiyejua ili aweze kujua na mgogoro upate kuisha
- Mgogoro unaweza kuwa kati ya mtu na mtu, mke na mume, au mtu binafsi au migogoro ya kisiasa n.k.
- Migogoro inafanya ngonjera ziwe na uhai na ziweze kutafakariana kiakili na kuamsha shauku ya utafiti unao ambatana na fikra.
- Kwa hiyo uti wa mgongo wa ngonjera ni migogoro na ngonjera nzuri zaidi iambatane na vitendo ili kuleta uhai zaidi na huleta msisimko katika uonyeshwaji.
(i) Lugha :
- Lugha ya ngonjera ni rahisi, sanifu na ni ya kisasa. Lugha ya ngonjera hushawishiwa na wakati tuliopo matatizo yanayo ambatana na mazingira pamoja na siasa ya nchi.
- Ngonjera huongeza msamiati katika lugha ya Kiswahili kwa wanao zisoma, kuzicheza, na pia kutilia mkazo katika lafudhi na kutamka vyema maneno ya Kiswahili.
- Fani hii inawasaidia wachezaji pia waangaliaji kukuza msamiati wao lafudhi. matamshi na ukakamavu katika kutumia lugha sanifu na rahisi kwa umma.
(ii) Mazungumzo ( mjadala )
- Ngonjera huwa na watu ambao hujibizana. Mhusika mmoja hutoa hoja ili ajibiwe na mwingine na mwandishi anayepaswa amwachie mhusika wake aonekane kwamba maneno anayoongea ni ya kwake mwenyewe siyo ya mwandishi. Na mhusika inambidi maneno anayo tumia yaendane na kile anachokiwakilisha. mfano: Daktari mvivu. Pia mjadala utusaidie kumjua mhusika tabia yake hisia zake mawazo yake, mazingira yake, wakati anaozungumzia na kutuonesha hali ya mchezo kiujumla.
(iii) Muundo
- Ngonjera Ina muundo ambao kama wa shairi ingawa kuna tofauti ndogondogo zinazo tofautisha ngonjera na shairi. Kutokana na muundo tunaona visa vinavyotiririka, vinavyojengwa kufikia kukua mpaka mwisho.
- Lazma mawazo ya mwandishi wa ngonjera yafuatane hatua kwa hatua yawe na mantiki na yaliyo na mtiririko wa fikra zenye kueleweka.
(iv) Vitendo
- Mara nyingi taswira au vitendo huanza kabla ya maneno vivyo hivyo misisimko inayotolewa na silka zilizojificha kama huzuni, furaha, huanza kuonekana kabla mtu hajaanza kuongea. Matendo yanatusaidia kufahamu anachofanya mhusika kwa sababu matendo na muondoko wa kulima ni tofauti na ya mwalimu n.k kwani hutofautiana jinsi ya kutumia macho, mikono, uso na hata jinsi ya kuweka mkazo na mlegezo.
- Vitendo hutasaidia kujua dhahiri dhamira za ngonjera yenyewe
(v) Jukwaa na vitu vinavyoonekana wakati wa kufanya ngonjera
- Tanzu yoyote ya fasihi simulizi huwa na mahali ambapo inatendekea na huitwa mandhari.
- Katika ngonjera pia huwa na mandhari ambayo yaweza kuwa shambani sokoni ukumbi wa mkutano kijijini au ndani ya nyumba, ofisini n.k. au inaweza kuchanganya mandhari mbili au zaidi kutokana na mwandishi alivyoamua kujenga kazi yake.
- Kwenye ngonjera kitu ambacho hutusaidia kujua mandhari ni maneno ya mhusika mwenyewe na maelezo ya mwandishi au kama linachezwa katika jukwaa ambalo jamii inaweza kuona maigizo hayo.
(vi) Mavazi ya wahusika wa ngonjera
- Mavazi ya wahusika katika ngonjera ni muhimu sana kwa sababu yatasaidia katika kufikisha ujumbe wa hadhira husika.
- Na pia yatatusaidia kutupa mwanga zaidi na kujua wahusika wetu na pia kutupa kazi na nafasi ya wahusika wa ngonjera hiyo.
- Na vilevile hutusaidia kujua vipindi mbalimbali ambavyo jamii imepita mfano; mavazi ya kipindi cha ukoloni wa kiarabu tofauti kati ya kizazi kimoja na kingine.
(vii) Mwanga na msaada wake katika kuonesha ngonjera
- Mwanga husaidia kuunganisha pamoja mambo yote yanoonekana jukwaani. Pia husaidia kuonyesha nguo wavaazo wahusika na vitu vyote vionekanavyo jukwaani na hata wahusika kuweza kuwaona waangaliaji wake.
- Na mwanga unaweza kuwa mwanga wa jua, mwezi, moto, taa za umeme, kibatari n.k.
- Hata hivyo mambo yote haya hutegemea na dhamira hiyo, ngonjera waonyeshaji na hata mavazi ya wahusika.
- Na pia katika ngonjera huweza kuambatana na muziki au ngoma hutegemea na ngonjera hiyo.
- Hali kadhalika muda mwingine huweza kuambatana na nyimbo fupi ambayo itasaidia kuonesha hali ya mchezo kwa ujumla, dhamira kusisimua n.k.
- Na muda mwingine nyimbo inaweza kufuata mwisho wa ngonjera
TOFAUTI YA MASHAIRI NA NGONJERA
S/N
MASHAIRI
NGONJERA
Shairi huweza kutungwa ili liimbwe kama vile redioni au lisomwe.
Ngonjera hukaririwa kwa maneno yenye kuonesha hali ya mazingira
Shairi huimbwa au kusomwa na mtu mmoja
Ngonjera husemwa na watu wawili au zaidi wanaojadili matatizo mbalimbali.
Maneno ya mashairi hutofautiana kutoka shairi hadi shairi, dini, majonzi, matatizo ya siku kwa siku
Maneno yake hulenga kujibu swali moja
- Mara nyingi mwisho wanangonjera huishia na mshindi na dhamira itakiwayo.
- Ni pia wakati mwingine watu huona kama udhaifu kwani inapasua pande zote mbili zijadiliwe kwa kina na kwa usawa. Upande wa kufaulu na kutokufaulu.
UANDISHI
Insha
- Ni mfululizo wa sentensi zinazohusiana na mada inayozungumziwa au kuandikwa. Uandishi wa insha huwa katika haya.
Kuna aina kuu mbili za insha
(a) Insha za wasifu
(b) Inshaza hoja
- Lakini pia insha hizi zinagawanyika tena mara mbili. Insha za wasifu za kisanaa na zisizo za kisanaa
- Insha za wasifu za kisanaa huwa na lugha ya mvuto na misemo kama nahau methali na tamathali za semi mbalimbali.
- Insha za wasifu zisizo za kisanaa. Ni insha ambazo huwa na lugha ya kawaida.
Insha za hoja
- Ni insha ambazo hutetea mawazo ya aina fulani na kupinga mengine kwa uthibitisho uliodhahiri. Insha hizi huonesha ubora na udhaifu wa mawazo yanayojadiliwa.
- Unapoandika insha za hoja hakikisha unapanga mawazo katika mtiririko unaofaa ili hoja zake zipate nguvu na kukubaliwa.
- Kunakuwa na pande mbili zinazopingana. Moja ikiunga mkono na moja ikikataa.
- Uelewa wa mada inayojadiliwa ni muhimu. Mwandishi awe na msamiati wa kutosheleza lugha sanifu na fasaha huku ukizingatia na sarufi ya lugha husika.
Hatua za uandishi wa insha
(a) Kichwa cha insha
- Hiki huandikwa kwa herufi kubwa katika juu na mara nyingi huwa hakizidi maneno matano (5). Kichwa cha insha huandikwa muhtasari kwa kuzingatia wazo kuu la insha na mara nyingi hupigiwa mstari.
(b) Utangulizi wa insha
- Huu huzingatia fasihi ya jambo linalozungumziwa, uhusiano wake na vitu vingine na muhtasari wa insha inayotungwa.
(c) Kiini cha insha
- Hii ndio sehemu kuu ya insha ambapo mwandishi anapaswa afafanue kwa mapana mada inayoelezwa huku akitoa mifano hai inayoendana na hali halisi. Kila haya huwa na wazo kuu moja.
(d) Hitimisho la insha
- Katika sehemu hii mwandishi anapaswa kutoa mapendekezo (maoni) ya msingi au kusisitiza. Kwa ufupi yale aliyoyaeleza katika habari yenyewe.
UANDISHI WA BARUA Barua rasmi - Hii ni aina ya barua ambayo huandikwa kwa makusudi maalum.
Dhima za barua rasmi
- Kuomba kazi au huduma
- Kuagiza na kupokea vifaa
- Kutoa taarifa mbalimbali kama vile kushindwa kufika mkutanoni kuomba kiwanja, mkopo
- Kutuma pongezi kwa aliyefanya vizuri kazini
Barua za kikazi zipo za aina nyingi lakini zinaweza kugawanywa katika mafungu matatu nayo ni: -
(a) Barua za taarifa
(b) Barua za maombi ya kazi/ huduma
(c) Barua za uagizaji na upokeaji wa vifaa.
- Barua za kikazi huandikwa kuelezea ujumbe maalum kwa hiyo huhitaji kuandikwa kwa makini na uangalifu wa kutosha. Ni muhimu kuandika waziwazi jambo lililokusudiwa.
- Mwandishi analazimika kuandika kwa ufupi na kwa lugha nyepesi, ni muhimu kuepuka maelezo yasiyo muhimu. Mara zote barua za kazi huwa na sentensi fupi, sentensi chache na zenye maana
MUUNDO WA BARUA YA KIKAZI
Anuani ya mwandishi
- Lazima mwandishi aandike anuani yake , iwe juu kwenye pembe ya mkono wa kulia wa karatasi. Hii inatakiwa iandikwe kikamilifu na kwa usahihi.
Tarehe
- Pia huandikwa mkono wa kulia wa karatasi barua, chini ya anuani ya mwandishi
Kumbukumbu namba
- Barua za kikazi ni lazima ziwe na kumbukumbu namba ya kuitambulisha. Mara nyingi kumbukumbu namba huwa na tarakimu au herufi au vyote kwa pamoja.
- Kumbukumbu namba hii ni kama jina la kutambulisha barua hiyo katika majibu au mfululizo wa majibizano
Anuani ya mwandikiwa
- Mara zote hutangulia na cheo cha mwandikiwa upande wa kushoto chini ya kumbukumbu namba. Nafasi kidogo huachwa baina ya kumbukumbu namba na anuani hii.
Mwanzo wa barua
- Katika sehemu hii ni heshima kutaja cheo cha mwandikiwa mfano; Ndugu katibu, Ndugu afisa mifugo, Ndugu mkuu wa shule, na huandikwa chini ya anuani ya mwandikiwa.
Kichwa cha habari
- Lazima barua ya kikazi iwe na kichwa cha habari kinachotaja kwa ufupi jambo linalohusu barua, kichwa cha barua huandikwa katikati ya barua mara baada ya mwanzo wa barua. Ni muhimu kiwe kifupi na chenye kueleweka waziwazi. Ni lazima kipigiwe mstari na kuandikwa kwa herufi kubwa.
Barua yenyewe
- Katika sehemu hii huandikwa mambo yote muhimu yanayohusu barua hiyo na taarifa zilizo dhamiriwa tu. Kwa sababu uanzaji wa barua yenyewe humrejesha msomaji kwenye maadili kufupisha maelezo kama vile: -
- Rejesha maongezi yetu ya juzi, mada hii inahusika, rejea mada hapo juu, barua yako ya tarehe.
Mwisho wa barua
- Sehemu hii ni tamko la heshima la kumalizia barua, mara nyingi mwisho unaotumika katika barua ya kikazi ni kama vile wako mtiifu, wako mwanachama/ mwanakijiji, wako katika ujenzi wa taifa, wako katika kazi n.k.
Saini na jina la mwandishi
- Mwisho wa barua mwandishi aweke saini na jina lake. Kama barua imechapwa basi itambidi aweke sahihi kwa mkono.
Cheo cha mwandishi wa barua
- Mwisho wa barua mwandishi aweke saini na jina lake kama vile katibu kata, waziri wa elimu, mjumbe wa shina.
BARUA ZA KIKAZI ZA TAARIFA
- Barua za kikazi za taarifa zinaweza kutoa taarifa fulani kama vile msiba, onyo, kushindwa kufika shuleni, mkutanoni, wizi uliotokea kijijini. Mara nyingi barua ya taarifa huweza kuwa na ombi.
- Ni muhimu kukusanya barua zote zinazohusu jambo hilo litamwelewesha kikamilifu anayeandika.
Mfano wa barua ya taarifa kuhusu “tatizo la simba kijijini''
Kijiji cha kafule
S. L. P 9
ITUMBA
20/08/1999
Bwana nyama ya Wilaya
S. L. P 10
ITUMBA
Ndugu;
YAH: TATIZO LA SIMBA KIJIJINI
Husika na kichwa cha barua hapo juu. Ninasikitika kukutaarifu kuwa hapa kijijini kwetu amezuka simba anayewinda watu. Ni simba jike na ana watoto watatu na ameonekana mara tatu hapa kijijini.
Simba huyo huingia hapa kijijini kutoka katika msitu wa hifadhi ya Taifa Ambasi. Tunaomba ruhusa yako tuweze kuweka mtego. Nitashukuru kama mtashauri jambo la kufanya mara utakapopata barua hii.
Wako katika kazi,
K.Makosi
Kamwene makosi
Mtendaji wa kijiji.
- Vile barua hii ya kikazi za taarifa wakati mwingine inaweza ikawa inatoa taarifa za mwaliko wa masuala mbalimbali kama sherehe, mkutano kuanzisha mradi fulani, kufungua jingo.
- Barua hii hueleza waziwazi kusudi la kuandikwa, tarehe, wakati mahali itakapofanyika. Mfano wa barua.
Shule ya Sekondari Buza
S.L.P 30 Tanga
10/09/2000
Mkuu wa shule
Wilaya ya Tanga mjini
S. L. P 300
Tanga
Ndugu,
YAH: OMBI LA MWALIKO WA KUKABITHI VYETI VYA KUMALIZA KIDATO CHA SITA (6)
Husika na kichwa cha habari hapo juu. Ninakualika uwe mgeni rasmi ili kukabidhi vyeti vya kuhitimu masomo ya kidato cha sita kwa wahitimu 600 katika shule ya Buza tarehe 20/09/2000. Kufika kwako ndiyo kufanikisha shughuli hiyo . sherehe hizo zitafanyika kwenye ukumbi wa shule hiyo kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni
Nitashukuru sana iwapo ombi letu litakubaliwa
Neeba Nsi Yomo
BARUA YA MAOMBI YA KAZI
- Barua hii inahitaji iandikwe kwa uangalifu zaidi. Huandikwa kwa ufupi na huandikwa mambo yaliyo muhimu tu mfano kiwango chako cha elimu.
- Kuna mambo mnne yanatakiwa kuzingatiwa wakati wa kuandika barua ya kuomba kazi nayo ni: -
(a) Kutaja kazi unayoomba
- Sehemu hii ni lazima mwandishi ataje bayana kazi anayoomba ili msomaji asipate shida kutambua aina ya kazi anayohitaji.
(b) Elimu na ujuzi
- Ni muhimu mwandishi kueleza sehemu na viwango mbalimbali vya elimu alivyonavyo na pia kutaja kwa majina ya shule pamoja vyuo alivyosoma.
- Vilevile ni vizuri kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi pamoja na nakala za vyeti vyako na hata kama cheti kinachothibitisha ujuzi wako.
(c) Maelezo binafsi kwa ufupi
- Ni muhimu pia kueleza mambo binafsi kama vile kuelewa umri kama muombaji ameoa au hajaolewa, vipaji alivyonavyo mwombaji au kama ana mambo mengine anayopendelea kama vile sanaa, uandishi, michezo, muziki.
(d) Wadhamini
- Pia mwombaji anapaswa kutaja majina ya watu ambao wanaweza kutoa taarifa zaidi kuhusu elimu tabia na hata ujuzi wake.
- Na watu hawa wanaweza kuwa waalimu wake wa shule au vyuo, mwajiri wake wa zamani,au kiongozi yoyote lakini ndugu au rafiki hairuhusiwi kuwa wadhamini.
BARUA YA UAGIZAJI NA UPOKEAJI VIFAA Mfano wa barua ya kupokea vifaa
Kijiji cha Mkwawa
S. L. P 180
Iringa
28/12/2000
Meneja wa kiwanda
Kiwanda cha zana za kilimo Mbeya
S. L. P 4000
Mbeya
Ndugu,
YAH: KUPOKEA VIFAA VYA KILIMO
Rejea barua yetu ya tarehe 15/12/2000. Ninayo furaha kukufahamisha kuwa vifaa ulivyotuma vimetufikia. Tumepokea vifaa vifuatavyo:
Majembe - 6
Toroli - 1
Slasha - 20
Mapanga - 10
Mashoka - 6
Vifaa hivi vikefika salama na viko katika hali nzuri na mradi umekwisha anza na tunakukaribisha kututembelea upatapo nafasi ili uone tunavyoendesha mradi huu
Wako katika kazi
P.Kaboka
Pambula Kaboka
Mratibu wa mradi
KADI ZA MIALIKO
- Hizi ni barua au kadi ziandikwazo kwa ajili ya kumualika mtu ahudhurie sherehe au kikao fulani.
- Jina la mwandishi na anuani yake
- Jina la mwandikiwa au mwalikwa
- Lengo la mwalikaji kwa ufupi
- Tarehe ya mwaliko
- Mahali pa kukutania
- Wakati wa kukutania
- Jibu lipelekwe kwa nani
UANDISHI WA BARUA ZA SIMU
- Simu za maandishi ni njia mojawapo ya mawasiliano ya haraka baina ya mtu na mtu. Mwandikiwa hupata taarifa haraka iwezekanavyo ukilinganisha na barua za kawaida.
- Taarifa ya simu ni fupi lakini ina ujumbe ulio wazi na unaoeleweka. Ufupi wa simu za maandishi unatokana na gharama kubwa za malipo kwa sababu gharama za simu hulipwa kulingana na idadi ya maneno yaliyoandikwa.
Barua za simu zipo za aina mbalimbali kama vile
(a) Barua za simu ya kawaida
(b) Barua ya simu ya kupeleka fedha
(c) Barua ya simu ya haraka
Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa barua za simu
Anuani ya mpelekewa habari
Anuani ya barua ya simu lazima iwe kamili na ya wazi kuwezesha barua hiyo kupelekwa kwa haraka iwezekanavyo bila matatizo. Pia anuani ya mji unapokwenda ni muhimu ikiwezekana na mtaa na namba ya nyumba
Taarifa au ujumbe
Mara nyingi ujumbe huwa na maneno machache pia habari ielezwe kwa ufupi mno na iwe inaeleweka lakini epuka maelezo yasiyo ya lazima.
Jina la mwandishi
Hakikisha unaandika kwa herufi kubwa barua yako ya simu
Kutoweka alama yoyote kama vile mkato, nukta n.k
Simu zenye taarifa zaidi ya moja zitengwe kwa kutumia nukta
Maandishi yote yanatakiwa yawe kwenye fremu.
Matumizi ya simu za maandishi ni kutoa taarifa mbalimbali kama:
Taarifa juu ya kifo, juu ya ugonjwa, taarifa juu ya kufaulu mitihani, kutoa taarifa juu ya kupata kazi, kutoa taarifa juu ya kujiunga na shule, taarifa juu ya safari n.k
Dhima za simu za maandishi
Kutoa taarifa za kilio, ajali au tukio lolote la ghafla kwa haraka, wazi, ufupi na huku zikieleweka.
Kupata majibu ya haraka
Hii ni pale kwa mtumiaji anapolipia majibu na kuandika maneno R.P (Reply paid) kabla ya jina la mpelekewa simu
Mfano wa barua ya simu
SHABANI MUSA SLP 54 KILIMANJARO NITUMIE 20000 YA MTIHANI PAMELA MISOSI
UANDISHI WA DAYOLOJIA
Dayolojia
- Ni mazungumzo au majibizano baina ya watu wawili au zaidi.
- Dayolojia yaweza kuwasilishwa kwa njia ya mazungumzo ya ana kwa ana au kwa maandishi.
- Katika utungaji wa dayolojia mtunzi hana budi kujifanya kama muhusika mwenyewe. Vilevile mtunzi anapaswa kutafakari kwa makini mada anayokusudiwa kuandika
- Pia anapaswa kutayarisha na kupanga mawazo kimantiki na kwa mtiririko wa kufurahisha wahusika. Hali kadhalika awapangie wahusika majukumu kulingana na matendo yao.
- Mfano kama mhusika ni mkulima basi lugha atakayopewa, vifaa hata mandhari iliyomo vifanane au viwe kama mkulima halisi.
Mambo ya msingi katika utunzi wa dayolojia
(i) Mazungumzo ya mhusika lazima yawe mafupi ili yakumbukwe na yasimchoshe msomaji au msikilizaji.
(ii) kutoa maelezo ya ufafanuzi katika mabano ili kumfahamisha msomaji na msikilizaji mambo yanayotendeka mfano (anasimama ghafla kwa hasira).
(iii) kutumia vihisishi mfano Lo! Ati!, kweli!, n.k ili kuifanya dayolojia iwe ya kusisimua.
(iv) Pawepo na mwingiliano wa mazungumzo ya wahusika na kudakia maneno ili dayolojia iwe na uhalisia mfano anaweza kutumia (.........)
(v) Lazima lugha inayotumika na mtunzi izingatie sarufi lakini lugha au maneno ya wahusika yatategemea shughuli walizopewa.
Mfano wa dayolojia
(Akiwa na uso wa hasira, mama anamwita binti yake)
Mama : (akiita) Rose, Rose!
Rose : Nini tena?
Mama : Njoo hapa haraka
Rose : (anakuja polepole) nimekuja haya sema
Mama : Nieleze ulilala wapi?
Rose : Mbona wewe sijakuuliza ulilala wapi?
Mama : Unasemaje?
Rose : kwani hukusikia, unataka faida
Mama : (anahamaki) kweli mtoto wewe ni ibilisi, shetani
Mkubwa................
Rose : Umemaliza matusi yako? Nitahama humu ndani
Mama : (amepiga mayowe ya hasira huku anamfukuza Rose)
Haya toka ndani na usirudi tena hata siku ya
mazishi yangu..............
Rose : (anamtazama mama yake kwa dharau) acha presha.
USIMULIZI WA MATUKIO
USIMULIZI
- Ni maelezo yanayotolewa kuhusu tukio au matukio yaliyotokea ambayo yanaweza kuwa mema au mabaya
AU
- Ni kitendo cha kutoa masimulizi juu ya mfululizo wa matukio yaliyotokea katika kipindi fulani cha maisha ya msimuliaji. Mada hii lengo ni kumuwezesha mwanafunzi kutumia lugha ya Kiswahili fasaha kusimulia matukio mbalimbali.
- Katika usimulizi wa matukio ni lazima kuwe na msimuliaji na msikilizaji. Msimulizi lazima awe na sifa zifuatazo.
(a) Msimuliaji anatakiwa aweze kuwasilisha masimulizi yake kwa namna itakayochangamsha hadhira yake na ili aweze kufanikiwa juu ya hili, msimuliaji anatakiwa awe na kiwango cha hali ya juu cha ubunifu.
(b) Msimuliaji lazima awe na ufahamu mpana na lugha ya utamaduni unaohusika – hii husaidia katika kuwakilisha ujumbe vyema
(c) Pia inabidi msimuliaji awe mcheshi na awe anajua jinsi ya kuutumia ucheshi katika kunasa hadhira yake. Ucheshi huo lazima uhusiane na kile kinachowasilishwa na hadhira inayohusika.
(d) Msimuliaji anapaswa kuzifahamu tabia za binadamu pamoja na kuielewa mikondo mbalimbali ya jamii, pamoja na kufahamu mahitaji ya hadhira yake kwa sababu hadhira ya watoto huwa na vionjo, lugha yake na hata matarajio yake.
(e) Msimuliaji anapaswa kuwa na uwezo wa ufafanuzi na anayefahamu mbinu zifuatazo za sanaa na maonyesho.
Ufafanuzi ni uwezo wa msimuliaji kuweza kuunda kugeuza na kuwasilisha kazi yake papo kwa papo bila ya kujiunga kwa muundo ni kama mabadiliko ya sauti, mikunjo ya uso n.k
Kuna mbinu mbalimbali zinazotumika katika usimuliaji wa matukio. Utendaji ambao huwa na sifa kadhaa ambazo ndizo huitwa mbinu za usimuliaji wa masimulizi. Mfano wa sifa mojawapo ni uongozaji na umalizaji wa masimulizi, mara nyingi uongozaji huwa na mianzo maalumu, hisia za wasikilizaji pia huonyesha kuwa ni mwanzo wa masimulizi.
Vilevile mwisho wake huweza kusaidia kupumzisha hadhira yake pia kama kuna mwasilishaji mwingine anayefuata huashiria kuwa anaweza akaanza kuhadithia.
Usimulizi wa matukio unasisitiza mtiririko mzuri wa visa pamoja na lafudhi sahihi ya Kiswahili. Pia usimulizi wa matukio huzingatia;-
(ii)Matamshi – ili msikilizaji aweze kueleweka na kusikika vizuri mzungumzaji hana budi kusema kwa sauti, kuweka msisitizo panapostahili, kupambanua kauli yaani kama ni kauli ya kuuliza aulize na kama kauli ya taarifa aiseme kama kauli ya taarifa.
(iii) Utumizi wa lugha- msimulizi hana budi kujua anayezungumza naye kinachozungumzwa wakati na mahali anapozungumzia ili kuweza kutumia maneno kwa ufasaha na sio vizuri kuchanganya lugha.
(iv) Urefu wa habari – ni vizuri basi masimulizi yakawa mafupi ili yasimchoshe msikilizaji.
(v) Uhakika wa yale yanayosemwa- kwa kawaida masimulizi huwa na ushahidi wa yale yanayosemwa. Hivyo huusisha mifano dhahiri, hoja za msingi na mapendekezo ya kusaidia kama kuna tatizo.
UFAHAMU
- Ufahamu ni ile hali ya kujua jambo na kuweza kulifafanua au kutoa taarifa zinazohusiana na habari hiyo.
- Ni kipengele katika lugha ambacho humpa msikilizaji mbinu za kueleza hicho alichozingatia, ufahamu hutokana na kusoma, kusikiliza na kutafakari jambo aliloliona, alilohisi au kugusa.
DHIMA YA UFAHAMU
(i) Husaidia kuokoa muda kwa kutoa taarifa mbalimbali kwa muhtsari.
(ii)Huweza kubadilisha tabia ya mtu baada ya kugundua mambo mazuri na mabaya katika maarifa au habari fulani
(iii) Humsaidia msomaji kutafakari kwa kina kutokana na habari au taarifa aliyosoma, aliyosikia au kuona (kuelimisha)
(iv) Huongeza ujuzi, maarifa na burudani kwa msomaji
AINA ZA UFAHAMU
(i) Ufahamu wa kusikiliza
(ii)Ufahamu wa kusoma
UFAHAMU WA KUSIKILIZA
Ni ule ambao mhusika anatoa taarifa hiyo kwa kusikiliza habari hiyo. Ili kuweza kupata taarifa au habari hiyo kwa njia ya kusimuliana lazima msikilizaji azingatie mambo yafuatayo: -
(i) Kuwa makini kwa kile kinachosimuliwa au kusomwa.
(ii)Kujua matamshi ya msomaji kuna watu ambao hawamudu kutamka matamshi sahihi ya lugha husika inabidi uyazingatie mfano loho badala ya roho, feza badala ya fedha.
(iii) Kuhusisha mambo muhimu na habari inayosimuliwa
(iv) Kubainisha mawazo makuu
Msikilizaji atalazimishwa kuwa katika hali ya utulivu, mawazo yako yote yanatakiwa kuwa katika mazingira hayo ili neno lisikupite
UFAHAMU WA KUSOMA
o Ni ule uelewa unaopatikana kwa njia ya kusoma. Msomaji huzingatia maana ya maneno, sentensi na habari yote.
o Msomaji pia huweza kutambua mpangilio wa herufi, maneno na tarakimu na kuzitofautisha. Pia huweza kuelewa maana ya misemo na nahau kulingana na jinsi zilivyotumika katika habari hiyo.
o Msomaji anahitaji kubuni mawazo makuu, maana ya maneno na misemo na kujibu maswali yatokanayo na habari aliyosoma.
Ufahamu wa kusoma hupatikana kwa njia ya
Kusoma kwa sauti
Kusoma kwa makini
Kusoma kimya
KUSOMA KWA SAUTI
Ni aina ya usomaji ambao humwezesha msomaji kupata ujumbe na kuweza kutamka kwa lafudhi ya Kiswahili sahihi. Usomaji huu wa sauti humsaidia msomaji ajisikilize na kujipima juu ya uwezo wake wa kutamka maneno inavyotakiwa na uwezo wa kuelewa yale anayosoma. Ni muhimu msomaji azingatie matamshi sahihi ya lugha ili apatie maana sahihi ya matamshi yenyewe mfano:- “alilima barabara ikapendeza sana” alikuwa na maana yaani njia lakini msomaji akisoma “alilima barabara ikapendeza sana” maana inayopatikana inakuwa sio njia kwa kuwa mkazo umetiwa pasipo staili.
Mfano tungo “mimina wewe” ititamkwa “mimi na wewe” inakuwa na maana tofauti na ile ya kitendo cha kumimina kitu kama maji. Badala yake itamaanisha mimi na pia wewe au sisi wawili kwa hiyo msomaji hana budi kukwepa athari za lugha nyingine katika usomaji wa Kiswahili mfano: lugha ya awali (kikabila) na lugha ya kiingereza.
KUSOMA KIMYA
Ni njia ambayo msomaji anapitisha macho kwenye maandishi kwa haraka bila mazingatio ya kina. Lengo la msomajini kupata maana ya jumla bila ya mazingatio na si ya undani. Usomaji wa namna hii hutumiwa sana na wasomaji magazeti au wasomaji wenye mambo mengi kwa muda mfupi na kupata alichokihitaji lakini ufahamu unaopatikana kutokana na njia hii ni wa juu juu
KUSOMA KWA MAKINI
Huu ni usomaji ambapo huvuta fikra zote kwa kile anachokisoma. Usomaji wa aina hii msomaji hana budi kuzingatia maana ya kila neno, sentensi na aya kwa makini. Ili kufanikisha usomaji wa namna hii muda, utulivu katika mawazo na mazingira yanayomzunguka msomaji ni muhimu. Nia kubwa ya kusoma kwa makini ni kupata uelewa kamili ili kujibu maswali, kufanya ufupisho n.k.
UPIMAJI WA UFAHAMU
o Baada ya kusoma ufahamu njia ya kumpima kama ameelewa au hajaelewa ni kumpa maswali. Kwa hiyo kujibu vibaya ina maana ya kwamba hujaelewa.
(a) Kubaini mawazo makuu
Mwandishi au msimuliaji akizungumza huwa na ujumbe anaotaka ufike kwa hadhira. Na wakati mwingine hupanga ujumbe huo kwa namna nyepesi ili msomaji na msikilizaji waelewane haraka .
Mara nyingine huchanganya mawazo zaidi ya moja kutoka aya moja lakini mawazo hayo huwa hayahusiani. Ni wajibu wa msomaji au msimulizi. Mfano wanafunzi wa shule yetu ni wakarimu, wanachapa kazi hodari. Tungo hii inamawazo mawili yaani ukarimu na uchapaji kazi
Mfano: -
Kila mtu ana lake, na tabu kuzidiana
Yatupasa tukumbuke, raha pia hupitana
Na hilo lifahamike, kwa urefu na mapana
Na tabu kuzidiana , kila mtu ana chake
Wazo kuu katika ubeti huu unaweza kuwa tabu na raha duniani, huzidiana baina ya mtu na mtu.
(b) Maana ya maneno na misemo
Katika habari ambayo mtu anapata katika kusikiliza au kusoma aghalabu kuna maneno magumu kwa hiyo maana ya maneno hupatikana kutokana na matumizi yaliyokusudiwa na kama msomaji atashindwa kupata maana itabidi atafute kamusi ya msamiati.
Mfano: -
“ Kwa muda mrefu mashirika ya umma yamekabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha, wakati mwingine baadhi ya mashirika haya yakiwa katika hatari ya kufilisika, katika kujaribu kuokoa serikali mara nyingi kuyapatia ruzuku au kuyaunganisha na yenye shughuli zinazofanana.
Katika mtiririko huohuo wakijaribu kuyapa uhai zaidi ambapo sasa yanaweza kupanga bei za huduma na bidhaa zao kwa lengo la kuyawezesha kujiendesha kibiashara badala ya kutegemea ruzuku. Tunatazama kwamba mashirika yote yatatumia vizuri fursa hii ili kujiimarisha kiuchumi ni bora kuzingatia ufanisi na kuepuka ubaadhilifu na wizi wa mali na fedha ndipo vyombo hivi vitaweza kujikwamua (kweli kweli)
Maneno magumu yaliyojitokeza katika kifungu hiki cha habari hii.
(a) Kufilisika
Ni ile hali ya mashirika ya umma kushindwa kuzalisha mali kiasi kwamba matumizi ya uzalishaji kuzidi mapato
(b) Ruzuku
Fedha zitolewazo serikalini kusaidia mashirika nje ya umma.
(c) Uhai
Misaada hasa ya kifedha itolewayo na serikali kwa mashirika kuondokana na tatizo la kufilisika
(d) Ufanisi
Hali ya utendaji wa kazi kwa ubora au maridadi zaidi.
(e) Ubadhilifu
Utumiaji mbaya wa mali ya shirika au serikali au kampuni n.k
KUFUPISHA HABARI
- Ni kitendo cha msomaji kubaini mawazo makuu katika kifungu cha habari kuunganisha mawazo yake kwa kutumia maneno yake mwenyewe.
- Lakini habari yenyewe huwa na maana sawa na ile ya awali ili msomaji kutumia maneno yake mwenyewe isipokuwa dhana ibaki ile ile.
- Mara nyingi habari inayofupishwa huwa theluthi moja ya habari ya awali (1/3 )
Matumizi
Hutumika wakati wa kutayarisha ripoti na kumbukumbu za mkutano.
Pia hutumika katika uhariri wa habari.
Husaidia kupata habari na kuokoa muda wa kusoma
Hutumika katika kuandika kumbukumbu za kila siku shijara.
Kuna hatua zinazotakiwa kufuatwa wakati wa ufupisho wa habari nazo ni: -
(i) Kusoma habari yote mpaka uielewe. Msomaji kabla ya kuanza awe amesoma habari yote na kuielewa kwa undani zaidi.
(ii) Pia inabidi achague taarifa na maneno maalumu yenye ( na habari ya asili) kabla ya kuanza kufupisha.
(iii) Lazima ulinganishe taarifa maalumu na habari ya asili.
(iv) Kuandika muktasari kama ilivyotakiwa.
(v) Linganisha usawa wa ufupisho na habari ya asili
Wakati wa kufupisha habari ni muhimu kuzangatia (njeo) wakati kauli nafsi kama ilivyotumika katika habari ya awali.
Ufupisho pia hujumuisha kuandika kichwa cha habari ambacho ni kiini cha habari yenyewe.
Kichwa cha habari huwa hakizidi maneno matano (5) baada ya kumaliza kufupisha hakikisha unaandika idadi ya maneno upande wa kulia chini na kufunga mabano
MATUMIZI YA KAMUSI
- Kamusi ni kitabu chenye maneno yaliyopangwa kwa utaratibu wa alfabeti na kutolewa maana na maelezo mengine.
- Kamusi huwa na idadi kubwa ya maneno ambayo hutolewa maana na maelezo yake kwa lugha hiyohiyo. Kamusi inayotumia lugha nyingine, ina maana kamusi hiyo inatumia lugha mbili tofauti. Mfano kiingereza na Kiswahili.
- Kamusi hutoa maana za maneno na pia huwa na methali, nahau, picha, ramani, michoro mbalimbali na vilevile huonesha matamshi ya maneno.
Muundo wa kamusi umegawanyika katika sehemu kuu tatu
(a) Mwongozo wa kamusi (utangulizi wa kamusi)
(b) Vifupisho na matumizi ya alama (sherehe ya kamusi)
(c) Kamusi yenyewe (matini ya kamusi)
MWONGOZO WA MSOMAJI
o Ni njia mojawapo inayolenga kumuelekeza mtungaji wa kamusi ili aweze kutumia kamusi hiyo bila kupata usumbufu.
o Katika sehemu hii ya mwongozo wa msomaji huusika na mambo yafuatayo:
(i) Taarifa zilizoingizwa kama vile vidahizo au vibadala vya vidahizo mfano benki (Tanzania) - bank (Kenya)
(ii)Inaweza ikawa kategoria za maneno mfano vielezi, nomino au vivumishi, vitenzi au umoja na wingi n.k
(iii) Pia inaweza ikawa maneno na matumizi ya hayo maneno
Mfano: -
Nomino (serufi)
Element (kemia)
Electronic (fizikia)
(iv) Mifano ya matumizi
Yapo maneno ambayo ili yatumike vizuri inabidi yafuatiwe na maneno au miundo fulani maalumu. Kutokana na hali hiyo ya upekee mifano ya matumizi imetolewa ili kumuelekeza msomaji jinsi atakavyotumia maneno hayo.
Mifano ya matumizi yapo katika italiki na imewekwa badala ya fasihi au sinonimu na kufunganishwa na nukta mbili pacha (:) kwa mfano baba
(v) Lugha kihenzo
Ni mtindo unaotumika kutolea fasili za vidahizo katika kamusi kwa ufupi, ufasaha na kwa utoshelevu na pia uwazi.
Mtindo huu hutumia alama zinazofupisha maelezo marefu au fasili mbalimbali.
UFUPISHO NA MATUMIZI YA ALAMA
agh
Aghalabu
taz
Tazama
ele
Elekezi
kv
Kama vile
fiz
Fizikia
ksh
Kishairi
kb
Kiboharia
kv
Kivumishi
kd
Kideni
kw
Kiwakilishi
kem
Kemia
kz
Kizamani
kh
Kihusishi
ms
Misemo
ki
Kiingizi
mt
Methali
kl
kielezi
nh
Nahau
km
Kwamfano
nk
Nakadhalika
kt
Kitenzi
nm
Nomino
ku
Kiunganishi
sie
Si elekezi
TARAKIMU ZA HERUFI
- Tarakimu kama (1,2,3,4,5) zimetumika kutenda maana za maneno.
- Tarakimu zilizo kwenye mabano ya mduara kama (1), (2), (3).
- Tarakimu zimetumika kutenda orodha ya misemo, nahau, methali.
- Tarakimu za kipeo kama paa1, paa2, paa3, paa4 zinazowekwa baada ya neno huonesha idadi ya vidahizo homonimu.
- Herufi zilizo kwenye mabano ya mduara kama (a), (b) hutumika kutenda maana tofauti za misemo au nahau.
HOMONIMU:
Neno lenye tahajia sawa na jingine lakini maana tofauti.
Mfano: kaka na kaka
TAHAJIA
Uwakilishaji wa sauti kwa herufi katika maandishi kufuatana na muendelezo wa maneno uliokubaliwa.
ALAMA (, )
Alama ya mkato inatenga
(a) Orodha ya sinonimu
(b) Mfuatano na minyambuo
(; )
Alama ya nukta mkato inatenganisha
(a) Fasili moja na nyingine ya vidahizo
(b) Fasili na sinomnimu ya kidahizo
(c) Kategoria moja na nyingine
(d) Misemo, nahau au methali na fasili
(e) Mfano mmoja wa matumizi wa mwingine.
(.)
Alama ya nukta
- Inatenga mzizi wa kitenzi na irabu ya mwisho
- Inatenga orodha ya (ms), (mf), (nh)
- Inatenga orodha ya minyambuo na taarifa zalizotangulia
- Kuonesha mwisho wa fasili ya kidahizo
(:)
Alama ya nukta mbili
- Huonesha kuwa kidahizo ni kiingizi
- Hutenga fasili na mfano wa matumizi
(!)
Alama ya mshangao
- Huonesha kuwa kidahizo ni kiingizi
[ ]
Mabano ya mraba
Hutumika kufungia alama za uelekezi wa kitenzi yaani elekezi (ele) au si elekezi (sie)
Alama ya mshale
Kuashiria vibadala
Alama ya mraba
Huonesha kurasa za majedwali mbalimbali
/ alama ya mkwaju
Inatumika kutenga maneno ambayo yanaweza kutumika moja au jingine katika nafasi hiyo kama enda/ piga mwayo au enda mwayo / piga mwayo
˜ alama ya mawimbi
Inaashiri
(a) Nafsi inayotakiwa kukaliliwa na kidahizo katika fungu la maneno au sentensi bila kurudia kukiandika.
Alama ya vidole
Huonesha kurasa za michoro mbalimbali
( ) mabano ya mduara hutumika kuonesha:-
(a) Vifupisho vya misemo, nahau, vitendawili na methali k.v, (ms), (mf) n.k
(b) Tarakimu za orodha ya misemo, methali na nahau kama vile (1), (2), (4)
(c) Vifupisho vya maneno ya matumizi kamavile (kb), (kz),(tiz), (km)
(d) Viambishi vya wingi wa nomino kama vile kiti (vi), mtu (wa) kwa nomino ambazo hufuata utaratibu wa kawaida na kupachika viambishi kwenye mzizi ili kupata wingi
(e) Umbo zima la wingi wa nomino kama vile mwizi nm (wezi) kwa nomino ambazo maumbo ya wingi hayafuati kanuni ya kawaida ya kupachika viambishi kwenye mzizi wa neno ili kupata wingi.
Kidahizo
- Ni neno lililoorodheshwa katika kamusi ili litolewa maana zake pamoja na taarifa nyinginezo. Vidahizo huorodheshwa kialphabeti na kuandikwa katika chapa iliyoko.
Kitomeo
- Kitomeo ni neno lililoingizwa katika kamusi kama kidahizo pamoja na taarifa zake zote kama vile kategoria, umoja (wingi), elekezi (si elekezi) n.k
Mpangilio wa vidahizo
- Kutokana na tofauti za kimuundo katika aina nyingine ya neno, kategoria, vidahizo huwekewa utaratibu maalumu katika kuingiza vidahizo hivyo.
- Jambo la msingi kuelewa ni kwamba vidahizo hupangwa na kufuata utaratibu wa kialfabeti A – Z
UMUHIMU WA KAMUSI KWA JAMII
Kamusi ina matumizi mengi kwa mtumiaji yeyote wa lugha. Hii ni kwa sababu zifuatazo: -
(i) Kamusi huonesha tahajia (spellings) sahihi za maneno
(ii)Kamusi hubadilisha aina ya neno
(iii) Kamusi huonesha (maana) fasili mbalimbali za maneno
(iv) Kamusi huonesha matamshi sahihi ya maneno
(v) Kamusi huonesha maarifa zaidi kuhusu lugha ya wazungumzaji
(vi) Kamusi huonesha alama na vifupisho mbalimbali vinavyotumiwa katika lugha husika
(vii) Kamusi huonesha asili ya neno. Mfano katika lugha ya kijerumani, kifaransa, kiajemi, kiarabu n.k
(viii) Kamusi husaidia kujifunza lugha ya kigeni kwani humsaidia msomaji kusoma na kuelewa matini zilizo katika lugha za kigeni.
Maana ya sherehe
Orodha ya maneno yaliyo kitabuni na yaliyoelezwa maana zote katika kurasa za mwisho wa kitabu.
UINGIZAJI WA VIDAHIZO
Katika lugha ya Kiswahili miundo ya maneno ya kategoria moja huwa tofauti na miundo ya maneno ya kategoria nyingine kwahiyo kutokana na tofauti hizo za kimuundo, maneno ya kategoria mbalimbali yameingizwa katika kamusi kama vidahizo kwa utaratibu maalumu kama ifuatavyo.
UINGIZAJI WA NOMINO
o Katika Kiswahili nomino huundwa na mzizi na kiambishi cha awali cha nomino kama mtu (mtu) kwa kawaida viambishi awali vya nomino,vinakuwa viwili, cha umoja na wingi mfano kiti/ vitu, mtoto/ watoto, mti/ miti
o Pia kuna baadhi ya vidahizo ambavyo maumbo yake ya wingi hayawezi kutabirika kwa urahisi mfano jino (meno), mwizi (wezi), mwiba (miiba), ukuta (kuta)
o Vilevile kama nomino umbo la umoja na wingi halikadiriki kamusi inaonesha umbo hilo moja tu.
UINGIZAJI WA KITENZI
Maumbo yote ya kitenzi huweza kubeba kiambishi awali “ku” kama vile kuandika, kucheza n.k. na kuingiza kwa mtindo huo hutegemea tungeweka vitenzi vyote katika alphabet “k” kwa hiyo kuepuka hivyo vitenzi vimeingizwa kwa kuangalia herufi ya kwanza ya mzizi wa kitenzi husika mfano andika, kucheza n.k
o Vitenzi vikiwekwa viambishi hutenga mzizi na irabu ya mwisho ya kitenzi mfano: pig – a, chez-a, lim – a, imb – a,. Nia ya kuweka hivi ni kuonesha mahali gani viambishi tamati vinatakiwa kupachikwa ili kupata mnyambuo.
UINGIZAJI WA VIVUMISHI
Vivumishi huundwa na mzizi na kiambishi cha upatanisho wa kisarufi cha niomino inayovumishwa kama m-zuri, wa-zuri, m –refu, m – safi. Kwa kuepuka maumbo mengi ya neno lilelile vivumishi vya aina hii vimeingizwa kwa alfabeti kwa kuangalia herufi ya kwanza ya shina lake kama zuri, - ema, - refu, na – safi n.k.
UINGIZAJI WA VIULIZI
o Haya ni maneno ya kuuliza jambo kama vile wapi? Gani? Nini? Lini? n.k maneno hayo yote huingizwa kwa alphabeti kwa kuangalia umbo la kwanza la kiulizi hicho.
o Katika kila kiulizi, msomaji anaelekezwa atazame pia na jedwali lake kupata maelekezo ya maana ya kuoneshwa maumbo ya ngeli nyingine maana hiyo hiyo.
UINGIZAJI WA HOMONIMU
o Ni neno lenye maana mbili au zaidi zinazokaribiana sana kama vile kupe nm
Mdudu mdogo anayeganda kwenye mwili wa mnyama na kufyonza damu
Mtu anayepata mapato bila kutumia jasho lake
o Neno kama hili huingizwa kama kitomea kimoja na maana zake kutengwa na namba.
UINGIZAJI WA VINYAMBUO
Kuna maneno ambayo yanapatikana kwa kupachika viambishi kwenye mzizi wa kitenzi nomino, vielezi na vivumishi mfano neno boresha kutoka kivumishi bora, taifisha kutoka taifa, neno zalisha, mzawa kutoka kitenzi zaa. Maneno kama hayo yenye maana tofauti na zile za maneno ya msingi au yanayotumika sana katika mazungumzo yameingizwa kwa kidahizo kamili.
UINGIZAJI WA KIDAHIZO CHENYE KATEGORIA ZAIDI YA MOJA
Kuna baadhi ya maneno yenye kategoria zaidi ya moja yaani huweza kutumiwa kama nomino au kivumishi. Kategoria zote mbili au zaidi huoneshwa katika kitomeo kimoja na kila kategoria huoneshwa taarifa zake. Lakini utaratibu huu hautumiki kwenye vitenzi kwa sababu vitenzi huwekewa vitone kutenganisha na mzizi na irabu ya mwisho wakati kategoria nyingine hazihitaji vitone. Mfano kadiri nm (maelezo) kl (maelezo).